Home Mchanganyiko ARUMERU YAPIGA MARUFUKU AJIRA ZA WATOTO WA MAJUMBANI( House Girl)

ARUMERU YAPIGA MARUFUKU AJIRA ZA WATOTO WA MAJUMBANI( House Girl)

0

*****************************

 

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro ametoa muda wa mwezi mmoja kwa wananchi wanaowatumikisha watoto wadogo kazi za majumbani (House Girls) kuhakikisha wanawpaleka watoto hao shule au kuwarejesha makwao

Dc Muro amesema endapo familia zinazoishi na watoto hao wa kazi wakishindwa  basi amewataka wawapeleke katika ofisi za Mkuu wa wilaya ya Arumeru ambapo Idara ya ustawi wa jamii italazimika kuwapeleka katika maeneo maalum ya kuwalea ili kuweza kupata fursa ya Elimu na malezi bora