JESHI la Magereza limekabidhi cheti maalum cha kuishukuru Benki ya NMB kwa msaada wa fulana ambao iliutoa kwa wanamichezo walioshiriki tamasha la michezo kati ya Magereza Bara na Vyuo vya Mafunzo Zanzibar.
Cheti hicho maalum kimekabidhiwa leo na Ofisa Michezo wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Matilda Mlawa kwa Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite ikiwa ni kutambua mchango wa benki hiyo mara kwa mara.
Akizungumza kwa niaba ya Jeshi la Magereza kabla ya kukabidhi cheti hicho, afisa huyo alisema wataendelea kujenga ushirikiano mzuri na benki hiyo kwa kuwa inawathamini hata maeneo mengine ya kijamii.
Kwa upande wake Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite alilishukuru Jeshi la Magereza kwa kutambua mchango na mahusiano mazuri kati ya pande hizo na kusema NMB itaendeleza ushirikiano huo. Aliongeza kwa sasa Benki hiyo imekuja na bidhaa bora zaidi ambazo wateja wao hasa taasisi zinazofanya biashara nao itafurahiya bidhaa hizo