Meneja wa Tigo Kanda ya Kusini Ladislaus Karlo (kushoto) akiongea na wananchi wa Sumbawanga wakati wa uzinduzi wa mnara wa 4G mjini Sumbawanga. Wa pili Kulia ni Katibu Tawala wa Manispaa ya Sumbawanga Christina Mzena akifuatiwa na Meneja Mauzo wa Tigo Rukwa Francis Ndada
Katibu Tawala wa Manispaa ya Sumbawanga Christina Mzena (kati kati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa mnara wa Tigo 4G wilayani Sumbawanga jana. Kushoto ni Meneja wa Tigo Kanda ya Kusini Ladislaus Karlo na kulia ni Meneja Mauzo wa Tigo Rukwa, Francis Ndada
Katibu Tawala wa Manispaa ya Sumbawanga Christina Mzena akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mnara wa 4G wilayani humo. Wanaoshangilia ni baadhi ya wafanyakazi wa Tigo waliohudhuria uzinduzi huo jana.
Katibu Tawala wa Manispaa ya Sumbawanga Christina Mzena akionyeshwa baadhi ya bidhaa za mawsiliano kama simu zenye uwezo wa G4 muda mfupi kabla ya uzinduzi wa mnara wa 4G uliofanyika jana. Anayemuelekeza ni Meneja Mauzo wa Tigo Rukwa Francis Ndada
********************************
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Tigo imezindua mtandao wenye kasi wa 4G mjini Sumbawanga,
utakaowawezesha wateja wake kupata huduma bora ya intanet, kupiga na kupokea simu, pamoja na ujumbe mfupi wa maneno (SMS).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mnara wa 4G mjini Sumbawanga, Meneja Tigo wa Kanda ya KusinI Ladislaus Karlo alisema mnara huo ulioongezwa ufanisi kutoka 3G kwenda 4G umeimarishwa ili kuweza kupitisha mfumo wa data kwa haraka zaidi, hivyo kuwezesha miamala ya fedha na huduma ya intanet kuwa ya kasi zaidi.
“Kama mnavyofahamu, Sumbawanga ni makao makuu ya mkoa wa Rukwa, hivyo
kupelekea mji huu kuwa kiungo muhimu wa shughuli za kiuchumi…hapa ndipo faida ya mtandao huu wa 4G unapoweza kudhihirika, katika kuwezesha biashara na kurahisisha upatikanaji wa taarifa na habari kwa kasi zaidi,” alisema Karlo wakati wa uzinduzi wa mnara huo mpya wa 4G.
Katika hotuba yake, Karlo alisisitiza pia kwamba wateja wa Tigo sasa wataweza
kutumia mtandao ulioimara, usiokuwa na vikwazo, ambao utawawezesha kufanya
shughuli zinazotumia kiwango kikubwa cha intanet, kama kutazama video, kusikiliza muziki, na kutuma na kupokea habari mtandaoni bila wasiwasi wowote.
“Wateja wetu wa hapa Sumbawanga ambao watahudumiwa katika eneo la mnara huu wa 4G watapata ofa maalum, watazawadiwa GB 4 za intanet bure pale
wanapobadilisha laini zao za simu kuingia 4G. Wateja wataweza kutumia kifurushi hichi cha intanet kwa muda wa siku 7,” alisema Karlo.
Karlo pia aliwakumbusha wateja wa Tigo Sumbawanga kuwa wanaweza wakapata ofa mpya ya ‘Saizi Yako’ ambayo inamwezesha kila mteja kupata ofa bora ya kupiga, kupokea simu, intanet na SMS iliyo mahususi na kuendana na mahitaji yao binafsi.
Kujiunga na ofa hiyo, piga *147*00# or *148*00#.”
“Kipaumbele chetu ni kuhakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma za teknolojia za kisasa kama vile mtandao wa 4G. Pia ni muhimu kutambua kwamba, teknolojia ya 4G imeongeza idadi kubwa ya watu kuunganishwa na intanet kupitia simu na pia imefungulia jamii zilizopo vijijini kuweza kupata huduma za kielektroniki katika nyanja za kibiashara, afya, elimu na serikali ambazo walishindwa kupata huko nyuma,” alisema
Karlo.
Mnara wa Sumbawanga ni wa nne kuzinduliwa baada ya uzinduzi wa minara iliyopo Mpanda, Katavi; Kilolo, Iringa na Bariadi. Jumla ya minara 52 itazinduliwa katika kampeni hii ya nchi nzima kwenye maeneo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kanda ya Ziwa, Kaskazini, Pwani na Kusini.