Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhandisi Stella Manyanya,akiwasili katika Ofisi za wizara hiyo zilizopo maeneo ya Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma leo. Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akisalimiana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhandisi Stella Manyanya,mara baada ya kuripoti katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo maeneo ya Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma akichukua nafasi ya aliyekuwa waziri Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akikumbatiana na aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Mhe. Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli kabla ya kukabidhi ofisi kwa Waziri huyo mapema leo jijini Dodoma.Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akisalimiana na watumishi wa wizara yake mara baada ya kuwasili kwa mara ya kwanza katika Ofisi yake tangu ateuliwe na Rais Magufuli kuchukua nafasi ya aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli leo amekabidhi ofisi hiyo.Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akiwa katika ofisi yake mpya akisaini vitabu mara baada ya kuwasili kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Rais Magufuli kuchukua nafasi ya aliyekuwa waziri Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli leo amekabidhi rasmi ofisi hiyo.Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli akitoa taarifa kabla ya kumkabidhi Ofisi Waziri Mpya Mhe.Innocent Bashungwa tukio hilo limefanyika katika Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma.Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akisikiliza hotuba ya aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa kabla ya kumkabidhi Ofisi tukio hilo limefanyika katika Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma.Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akikabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma leo.Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akiagana na aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli mara baada ya kumkabidhi Ofisi mapema leo hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma leo.Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli,akiagana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhandisi Stella Manyanya,mara baada ya kukabidhi Ofisi kwa Waziri Mpya Mhe.Innocent Bashungwa leo jijini DodomaWaziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa Wizara hiyo na aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli,mara baada ya kumkabidhi Ofisi mapema leo hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma leo.Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhandisi Stella Manyanya,akizungumza na watumishi wa wizara hiyo kabla ya kumkaribisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa.Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli,akisisitiza jambo kwa watumishi wa wizara hiyo wakati akitoa neno la kuwaaga na kumkaribisha Waziri Mpya Mhe.Innocent Bashungwa mara baada ya kumkabidhi Ofisi hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli,hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa,akisisitiza jambo kwa watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli,hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma.Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
………………..Na.Alex Sonna,DodomaWizara ya Viwanda na Biashara imesema kuwa kamwe haiwezi kushindwa katika utendajikazi huku ikitoa mambo muhimu kwa watumishi wake wanapaswa kuyazingatia katika kutimiza azma ya Rais Dk. John Magufuli, kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati.Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa,wakati akiongea na watumishi wa wizara hiyo baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Josephat Kakunda, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. Magufuli.“Siku zote siamini katika kushindwa na falsafa hiyo lazima ishuke kwa watumishi.”amesisitiza Mhe.BashungwaBashungwa amesema kuwa wizara hiyo ni muhimu katika kufikia azma ya kuifanya Tanzania kuwa taifa lenye uchumi wa kati ambao unatokana na maendeleo ya viwanda.Aidha Waziri Bashungwa ameyataja mambo matano ambayo ataanza kuyatilia mkazo na kuwataka wafanyakazi kushirikiana kutimiza majukumu ya kuwatumikiwa Watanzania.“Kwanza lazima tutumie fursa ya miundombinu iliyopo katika kuwezesha maendeleo ya viwanda. Rais ametoa mabilioni ya fedha kujenga reli, bwawa la kuzalisha umeme, barabara, umeme na mawasiliano.Hatua ya pili amesema kuwa ni kufanya utafiti utakaobaini mahitaji ya wakulima hususan katika kupata nyenzo za kilimo.“Katika hili, TIRDO, CARMATEC na SIDO mjiandae, serikali imeweka mipango mingi ya kuongeza uzalishaji kwenye kilimo, hivyo taasisi hizo zinapaswa kuja na mkakati wa kuwawezesha wakulima kupata nyenzo za kuboresha thamani kwenye mazao,” amesema Mhe.BashungwaAmetaja hatua ya tatu ni kubainisha ni kubaini utendajikazi wa viwanda vilivyobinafsishwa na vile ambavyo havifanyikazi, hatua zipi zinapaswa kuchukuliwa kwa wakati.Bashungwa amemalizia kwa kutaja hatua ya nne ni kuwepo ushirikiano baina ya idara za masoko na biashara kwenye wizara ya viwanda na ile ya kilimo.Aidha amewaomba watumishi kutekeleza mpango mkakati uliopo ili kuleta matokeo chanya kwa vitendo.Awali, Joseph Kakunda ambaye alikuwa waziri wa wizara hiyo, amesema kuwa katika kipindi cha utumishi wake amejifunza umuhimu wa Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo mara nyingi watu wamekuwa wakiilaumu na kuisifu.Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, amesema kuwa ni muhimu changamoto zilizobainika kwenye wizara hiyo zikatumika kama njia ya kuelekea kwenye mafanikio.Aliwataka watumishi kufanyakazi bila kukata tama kwa kumpa ushirikiano Waziri Bashungwa ili aweze kutimiza majukumu aliyopewa.