Home Mchanganyiko RC OLESENDEKA WASHUKIA WATENDAJI WA VIJIJI NA KATA WANAOKWAMISHA JITIHADA ZA TANAPA

RC OLESENDEKA WASHUKIA WATENDAJI WA VIJIJI NA KATA WANAOKWAMISHA JITIHADA ZA TANAPA

0

**************************************

NJOMBE

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wanaopiwa na ushoroba wa hifadhi za taifa Tanzania (TANAPA) Nyanda za Juu Kusini kuchukua hatua kali dhidi ya watendaji wa vijiji na Kata ambao wamekuwa kikwazo kwa Tanapa kuwapa elimu ya uhifadhi wa mazingira wananchi wanaoishi jirani na hifadhi za taifa.

Agizo hilo limetolewa na mkuu huyo wilayani Makete katika kijiji cha Magoye kata ya Itundu wakati wa mashindano ya uhifadhi wa mazingira ambapo zaidi ya watu 700 wameshiriki vikiwemo vikundi vya shule msingi na sekondari ambapo Olesendeka amesema serikali licha ya Tanapa kuongeza jitihada katika kuelimisha umma juu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira ya maeneo hayo muhimu lakini bado kuna watendaji wamekuwa kikwazo na kutoa agizo wote wa wilaya ya wakurugenzi.

Ruben Mfume mkuu wa wilaya ya Mbarali,Asia Abdalah mkuu wa wilaya ya Kilolo wakizungumza mara baada ya kukabidhi tuzo kwa wakazi walioibuka vinara katika mashindano ya uhifadhi wamesema serikali itaendelea kuwatambua washindi katika miaka mingine kwa kuwa inaongeza mshikamano baina ya umma na serikali katika kutunza mazingira ya hifadhi ikiwemo hifadhi za mto Ruaha.

Nao baadhi ya vinara akiwemo Kija Kiruki na Mariam Ngogo baada ya kukabidhiwa tuzo wanatoa mapendekezo yao kwa tanapa ambapo wanasema inapaswa kujenga mahusiano na jamii zinazozunguka hifahdi ili ziweze kulindwa