********************************************
Tarehe 31 Mei, 2019, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza kuwa ni
siku ya uteuzi wa wagombea katika Uchaguzi mdogo wa Udiwani
katika Kata Thelathini na mbili (32) za Tanzania Bara. Uteuzi huo
ulifanyika kama ilivyopangwa.
Katika Kata hizo Thelathini na mbili (32), jumla ya wagombea 98
kutoka katika Vyama kumi na nne (14) vya Siasa walishiriki
walichukua Fomu za Uteuzi. Vyama hivyo ni pamoja na AAFP,
UMD, ADA – TADEA, CCK, CCM, CHADEMA, CUF, DEMOKRASIA
MAKINI, NCCR – Mageuzi, NRA, SAU, TLP, UDP na UPDP.
Hadi muda wa mwisho wa uteuzi tarehe 31 Mei, 2019 saa 10: 00 jioni
kati ya wanachama 98 waliochukua fomu za uteuzi ni Wanachama 41
walirejesha fomu, kati ya hao 27 walikithi vigezo na kuteuliwa kuwa
wagombea na kupita bila kupingwa kutokana na kuteuliwa kwa
mgombea mmoja kwa kila Kata. Wanachama wengine watano (5)
hawakuteuliwa kuwa wagombea kutokana na sababu mbalimbali
ikiwemo kurejesha fomu za uteuzi nje ya muda, kukosa uthibitisho wa malipo ya dhamana na wagombea kuwa na idadi pungufu ya
wadhamini.
Jumla ya wagombea Watano (5) wa nafasi ya Udiwani waliwekewa
pingamizi kwa Msimamizi wa Uchaguzi na hivyo kupelekea
wagombea wawili (2) kuenguliwa kutoka katika orodha ya
wagombea wa nafasi ya Udiwani.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea Rufaa moja (1) kutoka kwa
Mgombea Udiwani wa Kata ya Ipole iliyopo Halmashauri ya Wilaya
Sikonge kupitia Chama cha Wananchi CUF, na malalamiko kutoka
kwa wagombea wa CHADEMA na CUF katika Kata ya Murangi
iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Malalamiko yao ni
dhidi ya maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi kuwaondoa kwenye
orodha ya wagombea udiwani.
Tume katika kikao chake kilichofanyika leo tarehe 4 Novemba 2019
kimetoa maamuzi kama ifuatavyo:-
Kwanza, Tume imekubali rufaa moja ya mgombea Udiwani wa CUF
katika Kata ya Ipole Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge na hivyo
kumrejesha kuendelea kuwa kugombea nafasi hiyo.
Pili, Tume imekubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi
katika Kata ya Murangi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ya
kumuondoa Wagombea wa CUF na CHADEMA katika orodha ya
wagombea na hivyo Wagombea kuendelea kuenguliwa kugombea
Udiwani.
Katika Uteuzi huu wa Udiwani katika Kata thelathini na mbili (32,
jumla ya Wagombea udiwani katika Kata 29 wamepita bila kupingwa,
na mgombea wa CUF kutoka Kata ya Kyaitoke Halmashauri ya
Wilaya ya Bukoba na mgombea wa ACT –Wazalendo kutoka Kata ya
Boma iliyopo katika Halmashauri ya Mji Mafinga wamejitoa kwenye
kinyang’anyiro hicho, hivyo Kata moja (1) ndio itakayofanya uchaguzi
hapo tarehe 17 Juni, 2019, kata hiyo ni Ipole Halmashauri ya Wilaya
ya Sikonge.
Kampeni za uchaguzi zimeshaanza kwa mujibu wa ratiba ya
uchaguzi na zitaendelea hadi tarehe 16 Juni 2019 ikiwa ni siku moja
kabla ya siku ya Uchaguzi.
Taarifa zaidi kuhusu walioteuliwa inapatikana kwenye tovuti ya Tume
ya Taifa ya Uchaguzi ya www.nec.go.tz na Ofisi za Tume Makao
Makuu.