**********************************************
Jay-Z ametangazwa rasmi na Jarida la Forbes kuwa ndiye bilionea wa kwanza wa Muziki wa HipHop huku akikadiriwa kuwa na utajiri wa jumla ya dola bilioni 1
Anamiliki hisa za dola milioni 70 kwenye kampuni ya usafiri ya Uber, dola milioni 70 kwenye masuala ya sanaa, dola milioni 50 kwenye umiliki wa majumba ya kupangisha na muziki, umiliki wa ‘Tidal’ inayouza nyimbo mtandaoni pamoja na umiliki wa Kampuni ya Roc Nation