kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire akionyesha kwa waandishi wa habari jana silaha aina ya SMG namba 260332 TZWD’KDU/IR/ 1990 mali ya KIDU inayodaiwa kuporwa kwa askari wa hifadhi ya Udzungwa Mwita Raphael (28) aliyeuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kabla ya kuporwa slaha hiyo na watu wanaodhaniwa na majangili

…………………..

Na Francis Godwin, Iringa

Jeshi  la polisi  linawashikilia watuhumiwa  wanne  kwa makosa mbali mbali  likiwemo la  kukutwa na meno ya  tembo  kamanda Bwire   alisema  kuwa   katika  tukio  la kwanza lililotokea  tarehe  1 june   katika     vijiji vya Mbawi  ,Masisiwe ,  Chita na  Ihimbo  jeshi la   polisi  kwa  kushirikiana  na kikosi   kazi  cha taifa  cha  kupambana na  ujangili  ,kikosi cha  kuzuia ujangili na  TFS – Tanza nia  Forest Service  walifanya  msako  wa pamoja  na   kuwakamata   watuhumiwa   wawili  pamoja na  silaha  aina ya SMG iliyoporwa  na watuhumiwa hao  wa ujangili .

Kamanda wa polisi  mkoa wa Iringa Juma Bwire amewaeleza leo  waandishi wa habari ofisini kwake kuwa  watuhumiwa hao wa ujangili   ndio  ambao  wamehusika la mauaji ya  askari  wa  hifadhi hya  Udzungwa  wilaya ya  Kilolo  Mwita  Raphael (28)  aliyeuwawa  kwa kuchomwa na  kitu chenye  ncha kali  /silaha kifuani na  kumpora  silaha  aina ya SMG  namba 260332 TZWD’KDU/IR/ 1990 mali ya  KIDU  ambayo imepatikana  na watuhumiwa hao  wawili .

Mbali ya tukio hilo  alisema  kuwa  watu  wengine  wawili  wakazi wa  kijiji  cha Wenda kata ya Tanangozi  wilaya ya Iringa  walikamatwa  na jeshi la polisi kwa  kushrikiana na afisa wanyamapori  walimkamata Geofrey Kiswaga (35) mkulima  akiwa na Nelson Kiduru (31)  wakiwa na meno ya Tembo  mamatu  yenye  uzito  wa 8Kg  ambayo thamani  yake bado kufahamika    waliyokuwa   wameyahifadhi  kwenye mfuko wa  salfeti kwenye  pikipiki  namba Mc 116 BMZ aina ya  Fekoni  iliyokuwa  ikiendeshwa na Kiduru  wakitokea  kijiji cha Nyamihumu Kidamali .

Kuwa  watu hao walikuwa  wakielekea kijiji cha wenda  kufanya  biashara ya  meno hayo kwa  wanunuzi  ambao  bado wanatafutwa na  jeshi  la  polisi .

Wakati huo   huo  jeshi la  polisi  mkoa wa Iringa  limewataka  wakazi wa mkoa wa Iringa  kuondoa  hofu  wakati  wa sikukuu ya  Idd kwani  jeshi la polisi  limejipanga  kuhakiisha  ulinzi na usalama  unawekwa katika maeneo yote ya starehe na ibada kwa  waumini wa  dini ya Kiislam.

 Kamanda  Bwire  alitoa onyo kwa madereva  wa pikipiki na vyombo vya moto kuendesha kwa  kuzingatia  sheria za usalama barabarani na  kuepuka  kuendesha  vyombo hivyo wakiwa   wamelewa  pombe  huku  akiwataka    wananchi  mkoani hapa kutoondoka  wote  majumbani kwao   kwenda  katika starehe   kwani kufanya  hivyo  ni  kukaribisha  wezi nyumbani .

Aidha  jeshi   la polisi mkoani Iringa  linamshikilia Jupista Mhinza  (30)  mkazi wa  kijiji cha  Kilolo  mkoani hapa kwa  tuhuma  za  kumchoma  na  kijinga  sehemu za  siri mtoto  wake wa  miaka    6  baada ya  kuchelewa  kurudi  nyumbani .

Kamanda  wa  polisi mkoa wa Iringa  Bwire  aliwaeleza waandishi wa habari jana  ofisini  kwake  kuwa  tukio hilo  lilitokea juzi   usiku katika kijiji cha  Kilolo  kata ya Kasanga  tarafa ya Kasanga  wilaya ya  Mufindi  ,ambapo mwanamke  huyo alichukua uamuzi  huo  baada ya  mtoto  huyo ambae ni mwanafunzi wa   shule ya msingi Kilolo  kuchelewa kurudi nyumbani .

 ” mtoto    huyo  alikuwa  akicheza na  watoto wenzake hivyo kuchelewa    kurudi nyumbani   kitendo  kilicho  mkwaza  mama mazazi na kuamua  kuanza  kumshambulia kwa  kipigo na kisha  kuamua  kumchoma na  kijinga cha moto  katika   sehemu  zake za  siri  na  kumjeruhi  vibaya ” alisema kama Bwire

Mtoto   huyo amelazwa  katika   kituo cha  afya Kasanga  akiendelea na matibabu na  mwanamke  huyo anashikiliwa na  jeshi la  polisi na  atafikishwa mahakamani kwa  tuhuma  hiyo ya  kumjeruhi  mtoto  huyo .