Home Mchanganyiko OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRA YAAHIDI KUTAFUTIA UFUMBUZI UPATIKANAJI MIFUKO MBADALA

OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRA YAAHIDI KUTAFUTIA UFUMBUZI UPATIKANAJI MIFUKO MBADALA

0

Afisa Mazingira Halmashauri jiji la Dodoma Bw.Ally Mfinanga, akizungumza na wananchi pamoja na wafanyabiashara wa soko la Majengo liliko jijini Dodoma Leo baada ya kutembelea na kujionea hali halisi ya utekelezaji pamoja na kuzindua kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.

Katibu Tawala wilaya ya Dodoma Bw.Edward Mpongolo akiongea na wafanyabiashara wa soko la Majengo liliko jijini Dodoma  baada ya kutembelea na kujionea hali halisi ya utekelezaji pamoja na kuzindua kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.

Meneja wa Kanda ya Kati kutoka Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) Bw.Carlos Mbuta,akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Majengo liliko jijini Dodoma  baada ya kutembelea na kujionea hali halisi ya utekelezaji pamoja na kuzindua kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.

Katibu Tawala wa Nkoa wa Dodoma Bw.Maduka Kessy,akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Majengo liliko jijini Dodoma  baada ya kutembelea na kujionea hali halisi ya utekelezaji pamoja na kuzindua kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.

Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Malongo,akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Majengo liliko jijini Dodoma  baada ya kutembelea na kujionea hali halisi ya utekelezaji pamoja na kuzindua kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.

Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Prof.William Mwegoha,akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Majengo liliko jijini Dodoma  baada ya kutembelea na kujionea hali halisi ya utekelezaji pamoja na kuzindua kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobas Katambi,akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Majengo  baada ya kufanya oporesheni ya kukagua huku akizindua kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobas Katambi,akiongea na mfanyabiashara wa mifuko mipya  baada ya kufanya oporesheni ya kukagua huku akizindua kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.

Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Malongo,akiangalia mifuko mipya ambayo imeanza kutumika nchi nzima mara baada ya kufanya oparesheni pamoja na uzinduzi kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.

Sehemu ya mifuko mipya ambayo imeanza kutumika leo kwa nchi nzima katika soko la Majengo na Sabasaba.

Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Malongo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobas Katambi,wakifanya oparesheni katika masoko ya majengo na sabasaba huku wakizindiua kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobas Katambi akimuonesha jambo Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Malongo,mara baada ya kufanya ziara ya Oparesheni na kuzindua  kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.

Sehemu ya wafanya biashara wa soko la Sabasaba wakifanya biashara zao za kuuza nyanya na baadhi ya bidhaa.

 Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Malongo,akinunua kikapu katika soko la Sabasaba mara baada ya kufanya ziara ya Oparesheni na kuzindua  kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobas Katambi akinunua kikapu katika soko la Sabasba akiwa na Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Malongo,mara baada ya kufanya ziara ya Oparesheni na kuzindua  kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.

Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog

………………….

Na ALEX SONNA,  DODOMA.

Katibu Mkuu Ofisi  ya Makamu wa Rais Mhandisi  Joseph Malongo, amewahakikishia wananchi kuwa ofisi yake inashughulia kwa ukaribu swala la bei ya mifuko mbadala ili kila mwana nchi aweze kuimudu.

Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma, wakati  uzinduzi wa   kikosi kazi maalumu cha kupambana na uharibifu wa mazingira kitaifa, amesema  ofisi yake inafanya jitihada  za kuhakikisha kila mwananchi anamudu garama za mifuko hiyo.

Amesema kumekuwa na malalamiko kuwa na uhaba wa mifuko mbadala na wengine wamekuwa wakilalamika kuwa bei ya mifuko hiyo sio rafiki, amebainisha kuwa wamekuwa wakihamasisha kuzalishwa kwa wingi mifuko hiyo.

“Kumekuwa na malalamiko kidogo kuhusu upatikanaji wa mifuko hii, na wengine wamelalamika kutokumudu garama sisi kama ofisi ya makamu wa raisi mazingira tunalitafutia ufumbuzi suala  hili ili mifuko ipatikane kwa wingi na kwa garama nafuu” amesema Malongo.

Amewataka wananchi kutokupuuzia sheria hiyo kwani sheria hiyo imetungwa kwa mujibu wa sheria za nchi, hivyo atakayepuuzia atachukuliwa sheria kali ambapo amesema kwa  watengenezaji faini milioni ishirini hadi bilioni moja.

Na kwa muuzaji ni faini ya shilingi laki moja ana isiyozidi laki tano au kifungo jela kisichozidi miazi 3 au vyote kwa pamoja, na kwa mtumiaji ni faini ya shilingi elfu therathini(30,000) au kifungo siku saba jela au vyote kwa pamoja.

Amesema kuanzia sasa ni marufuku mahala popote kutupa uchafu wa aina  yoyote ikiwa ni pamoja na kutumia mifuko ya plastiki, amebainisha kuwa kwa yeyote atakayekutwa na kikosi kazi anatupa  uchafu mahala masipotakiwa faini ni shilingi elfu hamsini.

Kwa  upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobus Katambi, amesema kuwa tangu katazo hilo lilipotangazwa na serikali wamekuwa wakizungukia maeneo mbalimbali wakitoa elimu na wananchi wamekuwa na mapokeo mazuri ya kampeni hiyo.

Amesema operation hiyo itakua endelevu na ametangaza kuwa ni marufuku kwa abiria yeyote kupanda kwenye daladala au pikipiki akiwa na mfuko wa plastiki, na amewataka makonda na madereva kuwa makini na abiria wanaopanda kwenye vyombo vyao.

Amesema  kuanzia sasa kila mtu katika nyumba yake ahakikishe anafanya usafi ndani ya mita 5 – 10, na kusipatikane mfuko wa plastiki katika maeneo yao na   yeyote atakayekutwa hajafanya usafi atachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha amewaonya wenye maduka ambao wamekuwa na tabia ya kutofanya usafi katika maeneo  yao watachukuliwa hatua za kisheria, na atakaye kutwa na taka katika nyumba atachukuliwa hatua za kisheria.

“Kwa suala hili  tumefanya vizuri tulipopokea tu taarifa ya katazo tulizunguka sehemu nyingi kutoa elimu ya masuala ya kutumia mifuko  mbadala na mapokea yalikuw ni makubwa sana, lakini wiito wangu ni kuhakikisha  kila mtu kwenye nyumba yake  ahakikishe ndani ya mita 5- 10 anafanyya usafi na kuondoa mifuko hiyo”, amesema katambi.