Home Michezo ESPERANCE MABINGWA WA AFRIKA,WAICHAPA 1-0 WYDAD CASABLANCA

ESPERANCE MABINGWA WA AFRIKA,WAICHAPA 1-0 WYDAD CASABLANCA

0

WENYEJI Esperance wamefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco bao pekee la mshambuliaji Mualgeria Mohamed Youcef Belaili dakika ya 41 akimaliia pasi ya kiungo Mtunisia, mzaliwa wa England Ayman Ben Mohamed Uwanja wa OlImpiki mjini Rades, Tunisia.
Kwa matokeo hayo, Esperance inayofundishwa na kocha Mtunisia, Moine Chaabani inabeba taji hilo kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Prince Moulay Abdallah mjini Rabat.
Siku hiyo, wageni Esperance wakitangulia kwa bao la dakika ya 44 la Fousseny Coulibaly kabla ya Cheick Comara kuisawazishia Wydad dakika ya 79, wafungaji wote raia wa Ivory Coast.

Wachezai wawili tu walionyeshwa kadi za njano usiku wa kuamkia leo, kiungo Muivory Coast, Coulibaly dakika ya 10 na Belaili dakika ya 42.
Hilo linakuwa taji la pili mfululizo kwa Esperance na la nne jumla kihistoria, baada ya awali kulitwaa katika miaka 1994, 2011 na 2018.
Kikosi cha Esperance kilikuwa; Rami Jeridi, Mohamed Ali Yakoubi, Anice Badri, Mohamed Youcef Belaili/ Hamdou Elhouni dk61, Taha Yassine Khnissi, Khalil Chamam, Fousseny Coulibaly, Saad Beguir, Ayman Ben Mohamed, Sameh Derbali na Franck Kom.
Wydad Athletic Club; Ahmed Reda Tagnaouti, Salaheddine Saidi, Ismail El Haddad, Aouk Badi, Walid El Karti, Aymane El Hassouni, Ayoub El Amloud, Yahya Jabrane, Abdelatif Noussir, Comara Cheick Ibrahim na Mohammed Nahiri.