Home Biashara BENKI YA BIASHARA YA DCB YAZINDUA BIDHAA MPYA YA AKAUNTI YA MUDA...

BENKI YA BIASHARA YA DCB YAZINDUA BIDHAA MPYA YA AKAUNTI YA MUDA MAALUM INAYOJULIKANA KAMA ‘DCB LAMBA KWANZA’

0

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB , James Ngaluko (wa tatu kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa akaunti mpya ya muda maalum ijulikanayo kwa jina la ‘DCB Lamba Kwanza’ inayomuwezesha mteja kupata riba ya hadi asilimia 14 papo hapo mara baada ya kuwekeza. Wengine kutoka kushoto ni; Meneja wa DCB Tawi la Temeke, Anna Kasyupa, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa, Meneja wa Akaunti za Kidigitali, Fredrick Mwakitwange na Meneja wa Tawi la DCB Magomeni, Fortunata Benedict.

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa (wa pili kushoto), akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa akaunti mpya ya muda maalum ijulikanayo kwa jina la ‘DCB Lamba Kwanza’ inayomuwezesha mteja kupata riba ya hadi asilimia 14 papo hapo mara baada ya kuwekeza. Wengine kutoka kushoto ni; Meneja wa DCB Tawi la Temeke, Anna Kasyupa, Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko, Meneja wa Akaunti za Kidigitali, Fredrick Mwakitwange na Meneja wa Tawi la DCB Magomeni, Fortunata Benedict

********************************************

Dar es Salaam, Mei 29, 2019.

Benki ya biashara ya DCB imezindua bidhaa maalumu
kwa ajili ya wateja wa akaunti ya muda maalum (Fixed Deposit) ijulikanayo kama ‘DCB LAMBA KWANZA’.

Bidhaa hii mpya itamuwezesha mteja wa DCB kuwekeza hadi miaka miwili na kupata riba ya hadi asilimia 14% ya amana atakayo wekeza na riba ya mwezi italipwa papo hapo pindi anapofungua akaunti.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa hii jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko alisema Akaunti hii itamuwezesha mteja wetu kupata riba kila mwezi hivyo kufanya wateja wa DCB kufurahia maisha kwani kila mwezi ni
mwezi wa faida.

“Riba inalipwa mwanzo wa mwezi kila mwezi, malipo ya riba ni rafiki mteja
anaweza kuwekeza kuanzia miezi mitatu (3) mpaka miaka miwili (2). Ni matumaini yetu wateja wetu watachangamkia fursa hii na watafurahia akaunti hii kwani tumeboresha maisha na uchumi”. Amesema Ngaluko.