Home Michezo ZAHERA ASHANGAZWA NA TAARIFA ZA AJIBU

ZAHERA ASHANGAZWA NA TAARIFA ZA AJIBU

0
Kocha wa klabu ya young Africa (Yanga) Mwinyi Zahera ameshangazwa na taarifa zinazosambaa juu ya aliyekuwa mchezaji wa klabu hiyo Ajibu Migomba kukwama kujiunga na timu yake mpya ya TP Mazembe.

“Sijui Ajibu yuko wapi, ila nasikia watu wanasema kwamba hatoenda tena Mazembe ataenda Simba, mara ataenda Yanga, mimi sijui”.  Amesema Zahera.

“Haitokei mara nyingi mchezaji kutakiwa na timu kama Mazembe au Al Ahly, na hata hapa Tanzania hakuna timu itamlipa kama ambavyo angelipwa na Mazembe, iwe Simba au Yanga”

“Labda kama ameangalia akaona akienda Mazembe hatocheza lakini Mazembe ni timu bora, ina miundombinu ambayo hata baadhi ya timu Ulaya haina. Mimi huwa nikienda Lubumbashi nashangaa mambo ya Mazembe” Ameongeza Zahera.