Home Mchanganyiko PROF. MCHOME ATOA MSAADA WA SHERIA KWA MWANANCHI MASWA

PROF. MCHOME ATOA MSAADA WA SHERIA KWA MWANANCHI MASWA

0

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome kulia akiwa wilayani Maswa mkoani Simiyu akiangalia nyaraka za Bibi Kang’wa Kija ambaye ni msimamizi was mirathi ya Kija Gogadi aliekuwa akihitaji msaada wa sheria baada ya suala hilo kuchukua muda mrefu bila ya kumalizika.

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome alievaa tai akisikiliza suala la Bibi Kang’wa Kija kutoka kwa mwanasheria wilayani Maswa ili kumsaidia mwananchi huyo ambaye ni msimamizi wa mirathi ya Kija Gogadi ambaye suala lake limechukua muda mrefu bila ya kumalizika.

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akipokea nakala ya Taarifa ya utendaji kutoka kwa Msaidizi wa Sheria kutoka wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipozungumza nao mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

WASAIDIZI wa sheria kutoka kituo cha msaada wa sheria wilayani Maswa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome na Msajili wa Watoa msaada wa sheria nchini walipokitembelea kituo hicho wilayani Maswa mkoani Simiyu

WASAIDIZI wa sheria kutoka wilaya za Maswa,Itilima na Meatu katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome na Msajili wa Watoa Msaada wa Sheria nchini walipokutana na wasaidizi wa sheria wa Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi.

………………………..

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome ametoa huduma ya msaada wa sheria wilayani Maswa mkoani Simiyu.

Prof. Mchome amemhudumia mwananchi Kang’wa Kija aliyemkuta kaika kituo cha Msaada wa sheria wilayani Maswa.

Bibi Kang’wa ambaye ni msimamizi wa mirathi ya Kija Gogadi amekuwa akishughulikia kwa muda suala lake bila ya kumalizika.

Prof Mchome amepitia nyaraka mbalimbali ambazo Bibi Kang’wa alikuwa nazo na kuzichukua kwa ajili ya kushughulikia suala lake.

Prof Mchome yuko mkoani Simiyu kwa ajili ya kukagua huduma za msaada wa sheria kwa wananchi kuona kama zinaendana na matakwa ya Sheria ya Msaada wa Sheria No.1 ya mwaka 2017.

Prof. Mchome pia amezungumza na taasisi zinazotoa msaada wa sheria na wasaidizi wa sheria mkoani Simiyu.

Kupitia mazungumzo hayo amewataka watoa msaada wa sheria kuendelea kufanya kazi hiyo kwa juhudi kubwa kwani Serikali iliwatambua kutokana na umuhimu wa huduma hiyo kwa wananchi huku ikizingatia uchache wa wanasheria nchini ili kuweza kutatua matatizo mbalimbai yanayowakabili wananchi nchini.

Amesema kutokana na uchache huo wa Wanasheria na ukubwa wa nchi ilikuwa inawawia vigumu kwa wananchi kupata huduma za kisheria nchini.

Amesema wasaidizi wa sheria  watasaidia kusuluhisha changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi  kama vile kupata haki zao, kumiliki mali na hivyo kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kuwa na jamii yenye afya na salama na kupata maendeleo.

Katika ziara hiyo Prof. Mchome  ameambatana na Msajili wa Watoa huduma ya msaada wa sheria nchini na msajili masaidizi kutoka katika Ofisi ya Mkoa wa Simiyu ambapo anatembelea vituo vinavyotoa msaada wa sheria na kuzungumza na wasaidizi wa sheria katika mikoa husika.