Home Michezo ASTON VILLA YAREJEA LIGI KUU UINGEREZA

ASTON VILLA YAREJEA LIGI KUU UINGEREZA

0

Aston Villa imerejea ligi kuu ya Uingereza baada ya kushuhudia timu hiyo ikiyeyusha matumaini ya kupanda daraja kwa kocha wa Derby Country ambaye ni mchezaji wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza Frank Lampard.

Aston Villa imerejea katika ligi hiyo baada ya kupata ushindi Wa bao 2-1 dhidi ya Derby County katika mechi ya fainali za play off iliyochezwa kwenye dimba la Wembley.

Villa sasa inaungana na Norwich na Sheffield United kucheza katika ligi kuu ya England msimu ujao.