Home Mchanganyiko WANAHABARI,WALIMU PAMOJA NA VIONGOZI WA DINI KUPATIWA ELIMU YA KATAZO LA MIFUKO...

WANAHABARI,WALIMU PAMOJA NA VIONGOZI WA DINI KUPATIWA ELIMU YA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI

0

***********************************

Kuelekea mwisho wa matumizi ya mifuko ya plastiki, wanahabari, walimu na viongozi wa dini watakiwa kupewa elimu ya katazo la mifuko ya plastiki ili wawezekutoa taarifa iliyokamili katika jamii kuhusu suala la katazo hilo.

Ameyasema leo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu katika Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari katika mkutano huo Mh. Samia amesema kuwa jamii inatakiwa wazoee kutumia mifuko mbadala kama vikapu mbalimbali ambavyo pia vimeshawahi kutumiwa na wazee wazamani kwani ni salama kwa matumizi.

“NEMC wanatakiwa kuharakisha kuwapatia vyeti wajasiliamali ambao wamejitokeza katika utengenezaji wa mifuko mbadala kuondoa usumbufu”. Amesema Mh. Samia Suluhu.

Aidha Mh. Samia amewataka viongozi wa kisiasa kutoweka zoezi la katazo la mifuko katika siasa kwani kunaweza kuwatengenezea bomu wananchi wake.

Hata hivyo Mh. Samia ameongeza kuwa kwa wale ambao wanauza maji kwenye mifuko(Kandoro) nao hawako salama kwani nao hutumia mifuko ya plastiki ambayo haitakiwi.

“Hilo suala halipo ikifika juni mosi hatutaki kuona maji yanayoitwa kandoro tena huko mtaani kwanza sina uhakika na usalama wa maji hayo”. Ameongeza Mh. Samia.

Kwa upande wa Waziri wa Mazingira Mh. January Makamba amesema kadri mifuko ya plastiki kuwa katika masoko basi mifuko mbadala haitakuwa rahisi kuingia katika masoko hivyo tujitahidi kuhakikisha tunatokomeza mifuko ya plastiki ili kuweka mazingira salama.

“Mpaka sasa wajasiliamali wengi wamejitokeza katika soko la mifuko mbadala hivyo tutaendelea kuwa nao sambamba kuhakikisha tunawaunga mkono”. Amesema Mh. Makamba.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda amesema kutokana na mkoa wa Dar es Salaam kuwa ndo kitovu cha matumizi ya mifuko ya plastiki kwa wingi basi watajitahidi kuzuia matumizi ya hiyo mifuko kwa kiasi kikubwa.

Pamoja na hayo Mh. Makonda amesema kuwa elimu ambayo inayoendelea kutolewa kwa wananchi kuhusu katazo la mifuko ya plastiki litakuwa endelevu katika jiji hilo hivyo wananchi wakifahamu basi utekelezaji wa suala hilo utakamilika