Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimpokea Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo, wakati Rais huyo alipokua amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa dharura akitokea nchini Afrika Kusini akielekea nchini Somalia. Katikati ni Balozi wa Somalia nchini, Mohamed Hassan Abdi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akizungumza na Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo, wakati Rais huyo alipokua amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo kwa dharura akitokea nchini Afrika Kusini akielekea nchini Somalia.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wa pili kulia) akimuaga Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo, wakati Rais huyo alipokua amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo kwa dharura akitokea nchini Afrika Kusini akielekea nchini Somalia.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kulia) akimpokea Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo, wakati Rais huyo alipokua amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa dharura akitoka nchini Afrika Kusini kuelekea nchini Somalia. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
RAIS wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam kwa dharura akitokea nchini Afrika Kusini kuelekea Somalia.
Akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, katika ukumbi wa mikutano wa Wageni Mashuhuri (VIP) uwanjani hapo, mara baada ya kupokelewa na Waziri huyo, Rais Farmajo alimpongeza Rais John Magufuli kwa kukuza uchumi na kuwa na uongozi imara katika nchi yake.
“Nina furaha kuingia Tanzania japo kwa dharura, kwa kuwa nchi hii ni Rafiki na Somalia, naomba mpelekee ujumbe huu mheshimiwa Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya, na pia mpe pongezi kwa kukuza uchumi,” alisema Rais Farmajo.
Rais Farmajo ambaye alitua nchini ajili ya ndege anayoitumia kuwekwa mafuta, pia alimuomba Rais Magufuli, nchi yake iweze kupata idadi kamili ya wazuiwa na wafungwa wote ambao wanakesi zinazohusiana na Uhamiaji waliopo magerezani hapa nchini, ili Serikali ya Somalia iweze kuwasafirisha kwa mujibu wa sheria.
“Serikali ya Somalia inatambua kuwa na uhusiano madhubuti na Tanzania, Somalia ipo tayari kufanya utaratibu wa kisheria ili kuweza kuwarudisha nyumbani wafungwa wote ambao wanakesi zinazohusiana na uhamiaji,” alisema Rais Farmajo.
Pia Rais Farmajo ameishukuru Tanzania kuwapa mazingira mazuri ya biashara, wafanayabiashara na Wawekezaji wenye asili ya Somalia walipo nchini.
Rais Farmajo aliwasili saa 8:38 mchana, jijini Dar es Salaam, na kufanya mazungumzo na Waziri Lugola kwa muda wa dakika 30, na baadaye aliondoka nchini kuelekea Somalia.