Home Mchanganyiko MADAKTARI ZAIDI YA 150 KUTOKA MATAIFA YA AFRIKA NA SEHEMU MBALIMBALI DUNIANI...

MADAKTARI ZAIDI YA 150 KUTOKA MATAIFA YA AFRIKA NA SEHEMU MBALIMBALI DUNIANI WANASHIRIKI KONGAMANO LA MADAKTARI WA MIFUPA

0

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akitoa hotuba ya
ufunguzi wa kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa mifupa
linalofanyika Tanzania (MOI) Kuanzia tarehe 26 -30 May 2019 katika ukumbi
mpya wa mikutano MOI

Madaktari wa Mifupa kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia mada katika
kongamano la kimataifa linalofanyika MOI

Madaktari wa Mifupa kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia mada katika
kongamano la kimataifa linalofanyika MOI

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza na
waandishi wa Habari (Hawapo pichani) katika kongamano la kimataifa la
madaktari bingwa wa mifupa linalofanyika Tanzania (MOI) Kuanzia tarehe 26
-30 May 2019 katika ukumbi mpya wa mikutano MOI

Mratibu wa Kongamano la Kimataifa la madaktari Bingwa wa Mifupa Dkt
Joseph Mwanga akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa
kongamano hilo.

*****************************************

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dkt Respicious Boniface leo
amefungua kongamano la kimataifa la madaktari wa Mifupa linalofanyika kwa siku
tano hapa Tanzania ambapo madaktari zaidi ya 150 kutoka mataifa ya Afrika na
sehemu mbalimbali duniani wanashiriki.

Dkt Boniface amesema Kongamano hilo limekua likifanyika hapa nchini kila mwaka
kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwapa mbinu mpya za matibabu ya mifupa
madaktari hapa nchini na nchi nyingine barani Afrika kutokana na MOI kuwa kituo
cha mafunzo kutokana na huduma bora za mifupa inazotozitoa.

“Madaktari bingwa wetu hapa nchini wamekua wakinufaika sana na kongamano
hili, wamekua wakipewa mbinu mpya na zakisasa za matibabu na upasuaji wa
mifupa jambo ambalo limepelekea MOI kuweza kumaliza rufaa za nje ya nchi kwa
wagonjwa wa mifupa ambapo kwa sasa huduma karibia zote zinapatikana hapa
nchini” Alisema Dkt Boniface.

Mratibu wa Kongamano hilo Dkt Joseph Mwanga amesema mafunzo yatatolewa kwa
njia ya nadharia, vitendo katika chumba cha maabara kwa kutumia mifupa bandia
na kwenda kwenye chumba maalum cha kujifunzia kwa kutumia miili ya binadamu
(Cadavers).

“Kongamano hili limekua na manufaa makubwa sana kwetu, tumekuwa tukipata
mbinu mpya kila mwaka kutoka kwa wenzetu wa Marekani jambo ambalo
limefanya huduma za mifupa hapa nchini ziendelee kuwa bora ukilinganisha na
mataifa mengine barani Afrika” Alisema Dkt Mwanga.

Kwa upande wake Profesa Michael Terry ambaye ni mkufunzi kutoka Chuo Kikuu
cha Calfonia cha San Francisco amesema ushirikiano kati ya Taasisi yake na MOI
umejikita katika mafunzo ya namna ya kuwahudumia majeruhi wa ajali kwa lengo
la kuwapa huduma bora na za kisasa kwa wakati.

Kongamano hilo limeratibiwa na Taasisi ya MOI kwa kushirikiana na Taasisi za
IGOT, SIGN, OTA, AO Alliance na Chuo kikuu cha Calfonia San Fransisco Marekani.