Home Mchanganyiko WANAFUNZI WAWILI SHULE SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA WATEULIKWA KULIWAKILISHA TAIFA KATIKA KONGAMANO LA...

WANAFUNZI WAWILI SHULE SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA WATEULIKWA KULIWAKILISHA TAIFA KATIKA KONGAMANO LA DUNIA

0

Mwenyekiti wa Halmashauri ya  wilaya ya  Mufindi mkoani Iringa Festo Mgina (kulia)  akiwakabidhi bendera ya Taifa  jana wanafunzi wa  shule ya  msingi Southern Highlands  Mafinga   kwa  ajili ya  wenzao  wawili   walioteuliwa kuliwakilisha Taifa katika  kongamano la mazingira  duniani  linalofanyika nchini Finland nkushoto kwake ni  mkurugenzi wa  shule  hiyo ambae ni  mkuu wa msafara wa wanafunzi hao Kitova Mungai.

WAnafunzi wa shule ya Msingi Southern Highlands Mafinga na walimu wao wakiwa zira ya kimasomo katika msitu wa Sao Hill Mufindi.

*****************************************

Na Francis Godwin, Iringa

Uongozi wa serikali ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa  umesema  umepokea kwa  heshima  kubwa mwaliko wa  wanafunzi  wawili  wa  shule  ya msingi  Southern Highlands  Mafinga   ambao  wamepata mwaliko wa   kuliwakilisha Taifa  nchini Finland katika kongamano la wanafunzi   dunia wanaojali  mazingira .

Akizungumza wakati akiwakabidhi bendera ya Taifa  wanafunzi hao na kiongozi wao  jana kwa  niba ya  serikali ya  wilaya ya wilaya ya  Mufindi  mwenyekiti wa  Halmashauri ya Mufindi Festo Mgina alisema kuwa  heshima  ambayo  shule  hiyo  ya  Southern Highnalnds  Mafinga  imepata  ni kubwa kwa  wilaya  ,mkoa na Taifa kwa  ujumla .

“Huu  ni  mwaliko  wa heshima  kubwa kwa wilaya  yetu na mkoa  lakini kwa Taifa  letu  kualikwa katika kongamano kubwa kama  hili  la  kujadili masuala ya mazingira  duniani  heshima hii sisi kama viongozi tunajivunia na tunapongeza  shule kwa  kuteuliwa kuwakilisha Taifa “  alisema  Mgina.

Kuwa  mwaliko  huo umekuja  wakati Taifa  liko katika  harakati ya kuhakikisha  mazingira  yanatunzwa na  kukabiliana na changamoto zinazoweza  kujitokeza kutokana na  mabadiliko ya tabia nchi  hata  kuanza mchakato  wa   kuondoa sokoni mifuko ya rambo ambayo ni moja ya  vikwazo  vya mazingira .

HIvyo  aliagiza  wakuu wa  shule za msingi katika  wilaya ya  Mufindi  kuhakikisha  wanafika katika shule ya Southern Highnalnds  Mafinga   ili  kujifunza  yale  ambayo  wanafunzi  hao wawili watarudi nayo kutoka katika mkutano  huo  mkubwa nchini Finland.

“tunataka elimu  na aagizo  ambayo yatatolewa katika  mkutano huo wa dunia nchini Finland  vijana hao  wakirudi  basi  kuweza  kusambaza kwa wenzao kwenye shule zetu  zote za MUfindi ikiwa ni pamoja na wakuu wa shule  kufika kujifunza  ili  kila shule kuweza  kujifunza  elimu  hiyo kwa faida ya  mazingira ya maeneo yao “  alisema Mgina .

KIongozi  wa  wanafunzi hao nchini Finland ,mkurugenzi wa  shule  hiyo  ya  Southern Highnalnds  Mafinga  Kitova Mungai  alisema kuwa    shule  hiyo ni miongoni mwa   shule wanachama wa  Klabu  za mazingira  duniani na  kuteuliwa kwa  wanafunzi hao   kumetokana na ziara ya   waratibu wa  kongamano  hilo ambao walifika  kupema uwezo  wa klabu zote  nchini .

Hivyo  baada ya  kuvutiwa na jitihada zinazofanywa na klabu ya shule    yake katika  utoaji wa elimu ya  mazingira  na  ufundishaji wa masomo ya  ujasiliamali  kwa wanafunzi  ndipo  wameweza  kutuma mwaliko  kwa wanafunzi  wawili na kiongozi  mmoja ambao  watakwenda  kushiriki kongamano hilo  kwa muda wa siku 10  safari ambayo itaanza jumanne wiki hii.

‘’ Tunategemea  kukutana na  wawakilishi  kutoka  nchi mbali mbali  duniani kama china ,Japan, Brazil ,Marekani ,China ,Uganda , Kenya  na nchi nyingine  nyingi ila  tunaimani kubwa ya  kuwakilisha  vema Tanzania kwani   watoto ambao wamechaguliwa  kwenda  katika kongamano  hilo  wanauwezo mkubwa sana katika  elimu ya mazingira “  alisema Mungai

Alisema  watoto hao  na  wenzao wamekuwa mbele  kuhifadhi mazingira ya Shule  ikiwa ni pamoja na uoteshaji wa miche ya miti  na  kuipata shuleni hapo na majumbani kwao  na  kwao  suala la  uhifadhi  wa mazingira  ni shughuli yao ambao  hata wakipewa nafasi ya kufundisha  wenzao wamekuwa wakifanya  vizuri.

Mungai alisema  kuwa  Tnzania ni imekuwa mbele katika  vita  dhidi ya mabadiliko ya Tabia nchi na  kuwa hata  mkakati wa serikali wa  kuzuia mifuko ya  rambo ni mkakati ambao  wanafunzi  hao   wamekuwa  wakifundishwa  namna ya  kutunza mazingira  pasipo  kutumia mifuko hatarishi ya mazingira  na kuwa kupitia kongamano hilo  watapata kuwasilisha mbinu mbali mbali za  utunzaji wa mazingira .

Kwa  upandev wao wanafunzi watakaowakilisha Taifa katika kongamano hilo Maria Wambura    na  Stephen  Sanga  ambao ni wanafunzi wa  darasa la saba katika  shule hiyo walisema   kuwa  kuteuliwa kwao  katika  kongamano hilo si nafasi ya bahati mbaya kwani wanauhakika  wa  kuliwakilisha  vizuri Taifa  katika  kongamano hilo na kile ambacho watakipata  watakuja  kutumia  kutoa elimu kwa wanafunzi wenzao nchini .