Home Mchanganyiko SPIKA NDUGAI AFUNGUA MAONYESHO YA MADINI KATIKA VIWANJA VYA BUNGE JIJINI DODOMA

SPIKA NDUGAI AFUNGUA MAONYESHO YA MADINI KATIKA VIWANJA VYA BUNGE JIJINI DODOMA

0

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akifungua maonyesho ya Madini yaliyoanza leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Maonyesho hayo yameanza leo tarehe 26 Mei, 2019 nakutegemea kumalizika kesho tarehe 27 Mei, 2019

Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo,akizungumza kwenye maonyesho ya Madini yaliyoanza leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Maonyesho hayo yameanza leo tarehe 26 Mei, 2019 nakutegemea kumalizika kesho tarehe 27 Mei, 2019

Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini,Prof. Shukran Manya,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa maonyesho ya Madini yaliyoanza leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Maonyesho hayo yameanza leo tarehe 26 Mei, 2019 nakutegemea kumalizika kesho tarehe 27 Mei, 2019

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Makamu wa Rais wa Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM), Ndg. Simon Shayo wakati alipotembelea banda ilo katika maonyesho ya Madini yaliyoanza  leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo, Maonyesho hayo yameanza leo tarehe 26 Mei, 2019 nakutegemea kumalizika kesho tarehe 27 Mei, 2019

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Kampuni ya K TanzGraphite, Ndg. Sauda Simba akimuonyesha na kumuelezea umuhimu wa madini ya graphite (kinywe) alisema utumika kutengenezea betri za simu, kompyuta mpakato ‘lap top’ na penseli wakati alipotembelea banda hilo katika maonyesho ya Madini yaliyoanza leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Prof. Yohana Msanjila na Meneja Maendeleo ya Jamii kutoka Kampuni ya K TanzGraphite, Ndg, Bernard Mihayo

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Meneja  Uhusiano wa Kampuni ya Utafiti ya madini ya Urani (MANTRA Tanzania), Ndg. Khadija Pallangyo akimuelezea kuhusu shughuli mbali mbali zilizofanywa na kampuni hiyo ikiwemo utengenezaji wa maktaba na uchimbaji wa visima wakati wa maonyesho ya Madini yaliyoanza  leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Uhusiano wa kampuni ya Shanta Gold Mine, Ndg. Christabella Hakili baada ya kufungua maonyesho ya Madini yaliyoanza leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo na Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Prof. Yohana Msanjila, Maonyesho hayo yameanza leo tarehe 26 Mei, 2019 nakutegemea kumalizika kesho tarehe 27 Mei, 2019,

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

…………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Serikali imewataka wachimbaji na wafanyabishara wa madini kuyatumia masoko ya madini ambayo yameanzishwa hivi karibuni katika Makao Makuu ya kila Mkoa  na kujiepusha na tabia ya kutorosha madini nje ya Nchi.

Hayo yamesemwa na Spika wa Bunge,John Ndugai,wakati akizindua Maonesho ya Madini katika Viwanja vya Bunge leo Mei 26,2019. .

Ndugai amewatahadhalisha wananchi wote wanajishughulisha na biashara na uchimbaji wa madini kuyatumia masoko ya madini ambayo yameanzishwa kila Mkoa  na kujiepusha na tabia ya kutorosha madini pamoja na magendo.

“Tumeona juhudi zinazofanywa na Rais Dkt.Magufuli za kuanzisha masoko ya madini na yamefunguliwa kila shemu ya nchi yetu na makao makii ya kila Mkoa”amesema Mhe.Ndugai

Spika amesisitiza kwa watu wanaojishughulisha na uzalishaji wa bidhaa za madini na bishara ya madini kuyatumia masoko hayo na kuwaonya waache na kujiepusha na  tabia ya kutorosha madini na magendo.

Spika Ndugai alisema Serikali kwa nyakati tofauti imekuwa ikifanya mabadiliko katika sheria na sera kwa nia ya kuhakikisha Taifa linanufaika na rasilimali ambazo zipo katika madini.

Aidha amesema kuwa kuna wakati tofauti Serikali  imekuwa ikifanya mabadiliko katika sheria  na sera kwa nia ya kuboresha yote hayo yamekuwa yakifanyika kwa nia njema ili kuhakisha Taifa linanufaika na shughuli za madini.na wadau wananufaika na shughuli za madini.

“Kumbukeni kuwa madini yakiishachimbwa yakaondoka hayarudi tena kwahiyo lazima hapa hapa kama kupata tupate hapa hapa sisi hawa hawa hakuna Kiswahili miaka ijayo”ameongeza

Spika amesema kuwa wote ni mashuhuda hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na serikali ya awamu ya tano na Bunge letu katika kodi ya zuio ya asilimia 5 kwa wachimbani wadogo pia kuna kodi ya ongezeko la thamani ya asilimia 18 ni vizuri hatua hizo zikahamasihwa zaidi

“Kwani baadhi ya Nchi jirani zimekuwa zikijinasibu kwamba ni wauzaji wakubwa wa madini, tunahitaji kusonga mbele hivyo ni lazima rasilimali madini tuliyojaaliwa na Mwenyezimungu tuhakikishe tunaisimamia ipasavyo,”amesema Spika.

Spika Ndugai amesema kuwa  Serikali itaendelea kuweka  mazingira mazuri

Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Madini,Mhe.Stanslaus Nyongo  amesema kuwa maonesho hayo ni muendelezo wa Wizara yake kuelimisha jamii juu ya shughuli zinazofanywa na Wizara yake pamoja na kutangaza fursa  zilizopo.

Mhe.Nyongo amesema kuwa  zaidi ya Makampuni 43 ya madini na Taasisi 7 zilizopo chini ya Wizara ya Madini zimejitokeza kushiriki maonesho hayo ambapo alidai kwamba leo Wizara yake inatarajia kuwasilisha bajeti yake.

“Kesho  tutawasilisha bajeti yetu naamini Wabunge wote watapa nafasi ya kujionea shughuli ambazo tunazifanya katika Wizara yetu,”amesema Nyongo.

Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini,Prof. Shukran Manya,amesema kuwa  wanamshukuru Rais,Dtk .John Magufuli kwa kutoa agizo la kuanzishwa kwa Masoko ya madini kwani kwa sasa kumekuwa na ongezeko la wananchi kwenda kuuza madini katika masoko hayo.

Aidha  Prof.Manya amesema kuwa kwa sasa kuna masoko 22 Nchini ambayo yamekuwa yakinunua madini ambapo kwa sasa mwitiko umekuwa mkubwa katika meneo ya Chunya na Geita.