Home Mchanganyiko POLEPOLE ATAKA MSHIKAMANO KWA WANA CCM WILAYA YA TANGA ILI KUPATA USHINDI...

POLEPOLE ATAKA MSHIKAMANO KWA WANA CCM WILAYA YA TANGA ILI KUPATA USHINDI CHAGUZI ZIJAZO

0
Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey
Polepole akizungumza wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akifuatiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee
 Sehemu ya wanachama wa
CCM wilaya ya Tanga wakifuaatilia kwa umakini hotuba ya
Katibu
Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa
Humphrey Polepole wakati wa
semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu
Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey
Polepole kulia akipokea tisheti ya umoja wetu ni ushindi wetu ya CCM
kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu
kushoto wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata
iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge huyo
katikati anayeshuhudia ni
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba

 Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey
Polepole wa pili kutoka kushoto akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo
kulia ni katibu wa CCM wilaya ya Tanga Salim Kidima ambaye
ameshikilia fedha zilizochangishwa kwenye semina hiyo kushoto ni
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba

 MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu ambaye pia ni
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akiwa kwenye
semina hiyo kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Tanga Salim Kidima akiwa
anahesabu fedha zilizotolewa

*******************************************

 
WANACHAMA wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga wametakiwa kujenga mshikamano na umoja miongoni mwao ili kuweza kuhakikisha wanakiwezesha chama hicho kupata ushindi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani.
 
Hayo yalisemwa  na Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata
iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu
(CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu.
Alisema lazima kuwepo mshikamano ambao utaawasaidia kuweza kuhakikisha wana kuwa wamoja kuelekea kwenye chaguzi zijazo ili kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuwatumikia watanzania kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.
Aidha pia katika semina hiyo  Katibu huyo alifanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Tanga ambapo jumla ya shilingi milioni 18 ziliweza kupatikana papo kwa papo huku Mbunge wa Viti Malumu (CCM) Mkoani Tanga ambaye pia Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akichangia shilingi milioni
5.
Sambamba na uchangiaji huyo lakini Waziri Ummy alitoa pia bendera za mashina 1000 na sare za chama ili kuimarisha chama ngazi za chini huku bendera 1000 za mabalozi na tisheti 800 ambazo watazitumia kwenye shughuli mbalimbali za kichama .