Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM, Dkt. Bashiru Ally, akieleza umuhimu wa elimu katika maendeleo ya jamii, wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM, Dkt. Bashiru Ally, akieleza umuhimu wa elimu katika maendeleo ya jamii, wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM Dkt. Bashiru Ally (katikati), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapher Shaaban (kushoto) na baadhi ya wadau wakifuatilia mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akimkabidhi zawadi Mtoto Summayya Juma, aliyeshiriki mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Baba Mzazi wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Mzee Abdalah Kijaji (katikati) na baadhi ya viongozi wa Dini Wilayani Kondoa wakifuatilia mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, wakizungumza jambo wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa dodoma Mustapher Shaaban, akieleza umuhimu wa elimu ya Dini katika kuleta umoja wa kitaifa, wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kulia), kwa jitihada za kuhamasisha elimu Jimboni kwake, wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Baadhi ya wanamashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma wakisikiliza wito wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM Dkt. Bashiru Ally (hayupo pichani), kuhusu kuwa wabunifu katika Nyanja ya Sayansi na teknolojia ili kuisaidia jamii inayowazunguka.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Pahi Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma wakishuhudia mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
*****************************************
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM Dkt. Bashiru Ally, amewataka watanzania
kutumia uwezo wa kuhifadhi Vitabu vitakatifu kuongeza ubunifu katika nyanja ya Sayansi na Teknolojia na nyingine ili kuendeleza jamii kwa kuipatia maendeleo stahiki.
Dkt. Bashiru ametoa wito huo katika Kata ya Pahi wilayani Kondoa mkoani Dodoma, wakati wa mashindano ya kuhifadhi Quran yaliyowashirikisha wadau kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa katika kuwekeza kwenye elimu kwa watoto, kwa kuwa watoto wakisoma si tu wanajengewa maarifa lakini pia wanaunganishwa na hivyo kuwa chachu ya kuweza kuisaidia jamii inayowazunguka.
Mratibu na Mwandaaji wa mashindano hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa lengo la mashindano hayo ya kuibua vipaji vya watoto vya kusoma Kitabu Kitukufu cha Quran na kuwajengea vijana uwezo wa kuwa na ujasili katika kueleza wanayo yaamini yakiwemo mambo mazuri ambayo yanafanywa na Serikali.
Kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia
Ackson, alisema kuwa kazi zinazofanywa na Dkt. Ashatu Kijaji, ni zakupigiwa mfano hasa kwa wanawake na akawataka wazazi katika Wilaya ya Kondoa kumuunga mkono kwa kushiriki kikamilifu katika mikakati ya kuinua elimu katika eneo hilo, kwa kuhakikisha wanawapeleka watoto katika makambi yaliyo na lengo la kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Mgeni Rasmi katika Mashindano hayo, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapher
Shabaan, amewapongeza vijana walioshiriki mashindano hayo na kuonesha umahili mkubwa wa kuhifadhi Quran na kuwataka waumini wa kiislamu kusoma na kukielewa kitabu hicho kitukufu kwa kuwa kimejaa elimu na maarifa mengi yatakayo wasaidia kuenenda vyema katika jamii na kupata thawabu kutoka kwa Mungu.