Home Mchanganyiko WAFANYABIASHARA NCHINI WATAKIWA KUBORESHA VIFUNGASHIO-BRELLA

WAFANYABIASHARA NCHINI WATAKIWA KUBORESHA VIFUNGASHIO-BRELLA

0

Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA)  Bakari Mketo akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kufika ofisi ya Forodha kituo cha Horohoro mpakani mwa Tanzania na Kenya wakati wa ziara yake wakati zoezi la Uhamasishaji wa utengenezaji wa bidhaa bora katika soko hilo ambapo alisema bidhaa bora ni lazima ziwe kwenye kifunganisho ambacho pia kitaonyesha taswira halisi ya thamani.

Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA)  Bakari Mketo kulia aakiteta jambo na Kaimu Afisa Forodha wa Kituo cha Horohoro Nsajigwa Mwambegele

Kaimu Afisa Forodha wa Kituo cha Horohoro Nsajigwa Mwambegele kushoto akiteta jambo na  Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA)  Bakari Mketo wakati wa ziara yake wakati zoezi la Uhamasishaji wa utengenezaji wa bidhaa bora katika soko hilo ambapo alisema bidhaa bora ni lazima ziwe kwenye kifunganisho ambacho pia kitaonyesha taswira halisi ya thamani.

Msajili Msaidizi Kitengo cha Ubunifu (Brella) Suzana Senso  akisisitiza jambo kwa Kaimu  Afisa Forodha wa Kituo cha Horohoro Nsajigwa Mwambegele katikati ni Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA)  Bakari Mketo

Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA)  Bakari Mketo katikati akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati wa ziara hiyo kushoto ni Msajili Msaidizi Kitengo cha Ubunifu (Brella) Suzana Senso kulia ni  Kaimu  Afisa Forodha wa Kituo cha Horohoro Nsajigwa Mwambegele

  Kaimu  Afisa Forodha wa Kituo cha Horohoro Nsajigwa Mwambegele katikati akiteta jambo kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA)  Bakari Mketo kulia ni Msajili Msaidizi Kitengo cha Ubunifu (Brella) Suzana Senso

Msajili Msaidizi Kitengo cha Ubunifu (Brella) Suzana Senso kushoto akitetaa jambo na Kaimu  Afisa Forodha wa Kituo cha Horohoro Nsajigwa Mwambegele wakati wa ziara hiyo

Msajili Msaidizi Kitengo cha Ubunifu (Brella) Suzana Senso kulia akiwa na Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA)  Bakari Mketo.

Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA)  Bakari Mketo katikati akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya ziara hiyo kushoto ni Afisa Mfawidhi wa Forodha wa Kituo cha Horohoro Bakari Athumani kulia ni Msajili Msaidizi Kitengo cha Ubunifu (Brella) Suzana Senso

Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA)  Bakari Mketo kulia akimkabidhi vipeperushi Afisa Mfawidhi wa Forodha wa Kituo cha Horohoro Bakari Athumani kushoto mara baada ya ziara hiyo

**************************************

WAFANYABIASHARA wa kati na wakubwa nchini wametakiwa kuboresha vifungashio vya bidhaa zao katika soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuepuka kupoteza ubora na bidhaa wanazotengeneza kutokana na kukosekana kwa hali hiyo.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA)  Bakari Mketo wakati alipofanya ziara ya kutembelea mpaka wa Horohoro unaotengenisha ya Tanzania na Kenya.

Ziara hiyo ilikuwa ni zoezi la Uhamasishaji wa utengenezaji wa bidhaa bora katika soko hilo ambapo alisema bidhaa bora ni lazima ziwe kwenye kifunganisho ambacho pia kitaonyesha taswira halisi ya thamani.

Aidha alisema kwamba lazima wafanyabiashara wahakikisha wanakuwa bora kwenye kuzipa thamani bidhaa zao kwani vifungashio sio kupaki tu bali hata ujumbe uliopo na nembo ya bidhaa anuani na eneo ambalo unapatikana ili kurahisisha upatikanaji wake.

“Isije kutokea watu wanakaa na vifungishio vya nchi jirani kuliko vya hapa nchini inafanya wakati mtu anaponunua bidhaa za ndani hajisikii kukaa na bidhaa hiyo kuliko ilivyokuwa vya nje kwenye soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo lazima tuingie kwenye ushindani tukiwa na ubora wa vifungashio”Alisema,

Mkurugenzi huyo alisema walichokuwa wakiangalia kwenye ziara hiyo ni namna gani brella wanaweza kupata huduma ya boda linki kwa kuhusanisha na kituo hicho cha horohoro ili kuhakikisha wadau wao hawapati usumbufu kwenye urasimishaji wa biashara zao .

Naye kwa upande wake Msajili Msaidizi Kitengo cha Ubunifu (Brella) Suzan Senso alisema mpaka sasa wamekwisha kutembelea mikoa 17 ambapo sehemu kubwa ya wafanyabiashara wamehamasika na kuanza kusajili biashara zao ili kukuza thamani ya bidhaa  wanazozalisha.

Alisema pamoja na mambo mengine watawaelimisha waafanyabiashara kuhusu mfumo wa usajili wa ORS hivyo wanaimani kubwa mwitikio wa wafanyabiashara kujisali utaongezekana kutokana na kupata uelewa wa masuala mbalimbali .