Makamu
mwenyekiti wa halmashauri hiyo Zakaria Vang’ota akiwa sambamba na
kaimu mkurugenzi wa
halmashauri ya Mji wa Mafinga Francis Maghembe
waalisema kuwa kupatikana
kwa hati safi katika Halmashauri hiyo kutachochea zaidi kasi ya utendaji kazi
ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa

 

 Baadhi ya madiwani na watendaji wa halmasahuri ya Mji wa Mafinga wakifuatilia kwa umakini ripoti ya CAG wakati wa baraza maalum la halmashauri hiyo

 NA FREDY MGUNDA,MAFINGA.

 

 

HALMASHAURI ya mji wa Mafinga imefanikiwa kupata
hati safi kutokana
na utendaji bora,usimamizi wa miradi ukusanyaji
mapato  kwenye vyanzo vyake vya ndani  katika kipindi cha
mwaka 2018-2019.

 

 

Akizungumza kwenye kikao maalumu cha  baraza
la madiwani wa halmashauri hiyo kwa lengo la kusoma rasmi taarifa  ya CAG kwa
niaba ya mkuu wa mkoa, Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Iringa, Lucas Kambelenje alisema
Halmashauri hiyo imeweza kupata hati safi katika kipindi cha mwaka 2018 -2019
kutokana na watendaji wake wakiwemo madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano
katika suala zima la kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa kiwango
kikubwa
ukilinganisha na kipindi cha nyuma.



‘’Nawapongeza
watendaji wa Halmashauri na madiwani kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na
kufanikiwa kupata hati safi, hivyo nawapongeza muongeze kasi zaidi kiutendaji
na kamwe msibweteke,’’alisema

 


Aidha aliwataka
kufuata misingi imara itayowawezesha kudhibiti mapato na
matumizi ya
halmashauri kwa kuondoa mapungufu yaliyojitokeza katika kipindi cha nyuma kama
kuchelewa kuwasilisha mahesabu kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za
serikali(CAG) ,kuchelewa kuwasilisha taarifa za matumizi  bila ya kuwa na
viambatanishi vya malipo .

 



‘’Pia epukeni
kulipa madeni hewa kwa watumishi ama  waliokufa,kuacha kazi
ama
watumishi watoro sehemu za kazi, kwani kufanya hivyo kutapelekea halmashauri
kupata hati chafu.

 


Kwa upande wake makamu
mwenyekiti wa halmashauri hiyo Zakaria Vang’ota alisema kuwa kupatikana
kwa hati safi katika Halmashauri hiyo kutachochea zaidi kasi ya utendaji kazi
ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.

‘’Ni dhahiri kila
diwani atatekeleza majukumu yake ili kuweza kudhibiti mapato na matumizi ya
halmashuari ma kuweza kufanya vizuri zaidi,‘’alisema Vang’ota.

 



Hata hivyo Vang’ota
aliwahimiza madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano na kuepuka kufanya kazi kwa
mazoea na kuwataka kuwatendea haki wananchi ambao wamewachagua kwa kuhakikisha
maendeleo yanawafikia wananchi kwa kuwatataulia kero zinazowakabilia.

 

 

Akizungumzia hoja hizo kaimu mkurugenzi wa
halmashauri ya Mji wa Mafinga Francis Maghembe alisema kuwa watahakikisha hoja
zote zinafanyiwa kazi ili kusijitokeze hoja nyingine au kuongezeka kwa madeni
ambayo halmashauri inadaiwa.