Home Mchanganyiko Mkutano wa siku mbili wa Maofisa TEHAMA (ICT) wa Wizara...

Mkutano wa siku mbili wa Maofisa TEHAMA (ICT) wa Wizara ya Afya wafunguliwa leo

0

Mkurugenzi wa Sera na Mipango ambae pia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bw. Edward Mbanga akifungua Mkutano wa Wataalamu wa TEHAMA (ICT) wa Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma uliofanyika leo Jijini Dodoma.

Mkurugenzi anaesimamia viwango, usalama na miongozo ya TEHAMA (EGA) Bw. Moses Makoko akiwasilisha mada mbele ya jopo la Wataalamu wa masuala ya TEHAMA (ICT) kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma katika kikao cha siku mbili kilichofanyika jijini Dodoma ili kujadili changamoto na mapendekezo ili kuboresha utendaji kazi wao.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango ambae pia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bw. Edward Mbanga akisema jambo mbele ya Maofisa TEHAMA kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma katika kikao cha siku mbili kilichofanyika jijini Dodoma ili kujadili changamoto na mapendekezo ili kuboresha utendaji kazi wao. Kushoto kwake ni Mkurugenzi anaesimamia viwango, usalama na miongozo ya TEHAMA (EGA) Bw. Moses Makoko na kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Afya Bw. Walter Ndesanjo.

Jopo la Wataalamu wa masuala ya TEHAMA (ICT) kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma wakifuatilia kwa karibu ujumbe kutoka kwa Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Sera na Mipango ambae pia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bw. Edward Mbanga

Picha zikionyesha Jopo la Wataalamu wa masuala ya TEHAMA (ICT) kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma wakifuatilia kwa karibu ujumbe kutoka kwa Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Sera na Mipango ambae pia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bw. Edward MbangaJopo la Wataalamu wa masuala ya TEHAMA (ICT) kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma wakifuatilia kwa karibu ujumbe kutoka kwa Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Sera na Mipango ambae pia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bw. Edward Mbanga

Jopo la Wataalamu wa masuala ya TEHAMA (ICT) kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma wakifuatilia kwa karibu ujumbe kutoka kwa Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Sera na Mipango ambae pia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Bw. Edward Mbanga

Picha ya pamoja ikiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya ambae pia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Edward Mbanga baada ya kufungua kikao cha siku mbili cha Maofisa TEHAMA (ICT) kutoka Wizara ya Afya na Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma kilichofanyika jijini Dodoma ili kujadili changamoto na mapendekezo ili kuboresha utendaji kazi wao.

……………………………………………………………..

Na WAMJW- Dom

Mkutano wa siku mbili wa Maofisa TEHAMA (ICT) kutoka wa Wizara ya Afya, Taasisi zake pamoja na Hospitali za Mikoa na Mabalaza ya kitaaluma umefunguliwa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Edward Mbanga Jijini Dodoma.

Lengo la Mkutano huo ni kupitia miongozo ya matumizi sahihi ya TEHAMA Serikalini ili kuongeza ufanisi wenye tija katika matumizi ya TEHAMA utaosaidia kuboresha utoaji huduma katika Sekta ya Afya nchini.

Mbali na hayo kikao hicho kimelenga kupitia mbali mbali wanazokumbana nazo Wataalamu hao katika utoaji huduma na kutoa mapendekezo ya kutatua changamoto hizo ili kuboresha utendaji wao katika Sekta ya Afya.

Hata hivyo kikao hicho kilichowakutanisha Wataalau wa masuala ya TEHAMA kimekusudia kujenga uelewa wa pamoja baina ya Wataalamu hao hususan katika masuala ya Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo na matumizi sahihi ya TEHAMA Serikalini.

Kwa upande mwingine Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya ambae pia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Edward Mbanga amepongeza uwepo wa mkutano huo jambo litalosaidia kuiboresha zaidi taaluma hiyo, hovyo kuahidi kumwalika Afisa Mwandamizi wa Idara ya Utawala ataesikiliza na kutatua changamoto zinazowakumba.