Home Mchanganyiko DKT.GWAJIMA AKERWA NA KASI YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA ILONGERO...

DKT.GWAJIMA AKERWA NA KASI YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA ILONGERO SINGIDA

0

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia afya, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Dorothy Gwajima akiwasili katika eneo linapojengwa Hospitali ya Wilaya ya Ilongero, Mkoani Singida kukagua  ujenzi wa Hospitali hiyo mpya ya Wilaya.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia afya, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Dorothy Gwajima akikagua  ya Jengo maabara linalojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ilongero, Mkoani singida

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia afya, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Dorothy Gwajima akisikiliza maelezo kutoka kwa viongozi wa Mkoa wa Singida kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Ilongero, Mkoani Singida.

Naibu Katibu Mkuu Afya, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Dorothy Gwajima  akikagua jengo la maabara linalojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ilongero Mkoani Singida.

Jengo  la mionzi ambalo lipo katika hatua za msingi linalojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ilongero, Mkoani Singida

……………………

Na. Angela Msimbira SINGIDA

Naibu Katibu Mkuu Afya kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Dorothy Gwajima amesikitishwa na kasi ndogo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ilongero, Mkoani Singida.

Akiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Ilongero iliyoko Mkoani Singida Dkt. Gwajima amesema ujenzi wa Hospitali hiyo unaenda kwa kasi ndogo jambo ambalo litasababisha kurudisha nyuma juhudi za Serikali za kukamilisha ujenzi wa Hospitali za Wilaya Nchini ifikapo Juni, 2019 ili ziweze kuanza kutoa huduma kwa jamii.

Amesema kuwa, majengo ambayo yameshafikia hatua ya lenta ni majengo matatu kati ya saba yanayotakiwa kukamilika kufikia tarehe 30 Juni, 2019 kama ilivyoagizwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo kuwa, Halmashauri 67 zinazojenga hospitali husika zihakikishe zinakamilisha  ujenzi huo ifikapo tarehe hiyo.

“Inasikitisha kuona baadhi ya majengo kama jengo la mionzi, maabara na huduma za uzazi bado yapo katika hatua ya msingi, hivyo naukumbusha  Uongozi wa Halmashauri kuwa, maagizo ya Mheshimiwa Waziri ya tarehe ya kukabidhi majengo hayo yakiwa kamili na bora haijabadilishwa na ni tarehe 30 Juni 2019”. Amesisitiza Dkt. Gwajima.

Amesema kuwa inasikitisha kuona kasi imekuwa ndogo licha ya serikali kuwa imetoa fedha zote tangu mwaka jana Oktoba 2018 na wataalamu wapo ambao, walitakiwa kuweka mipango vizuri na kudhibiti changamoto ambazo zingetarajiwa kujitokeza kwa kuwa na mpango mbadala.

Dkt.  Gwajima amesema, kutokuwa na mpango mbadala wa kudhibiti changamoto zinazoweza kujitokeza ni kikwazo katika utekelezaji, hivyo sijaridhishwa  na sababu zilizotolewa na anaamini zingeweza kudhibitiwa iwapo kungekuwa na mpango mbadala.

Aidha ameuagiza  uongozi wa Mkoa wa Singida kuhakikisha wanasimamia ujezi wa Hospitali hiyo kwa weledi mkubwa, wakizingatia viwango na dhamani ya fedha inayotumika iendane na majengo yanayojengwa na ujenzi  ukamilike kwa wakati kama ilivyoagizwa na Mhe. Sulemani Jafo.