Na Mwandishi wetu
VINARA wa soka katika michuano ya Ligi Kuu ya Hispania, LaLiga, timu ya Sevilla FC inatarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Simba ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya kwa timu hiyo kucheza nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam, timu hiyo inatarajiwa kuwasili kesho jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
Kulingana na taarifa hiyo mechi hiyo itakuwa ni maalum kwa vinara hao wa ‘LaLiga ambao wanadhaminiwa na SportPesa’ na akaongeza kwamba ziara itahusisha matukio kadhaa ya jamii na michezo ikiwemo kliniki namafunzo mbalimbali.
“Kama ushindani wa kimataifa unakutana na dhamira ya LaLiga kuwa karibu na mashabiki wake.
Kwa kweli kwamba mashabiki wetu wa Tanzania wataweza kupata furasa ya kuangalia karibu klabu kubwa kama Sevilla FC inamaanisha kuwa ni fursa kubwa kwa kila mtu,” alisema Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kimataifa katika Ligi ya La Liga, Oscar Mayo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Tarimba Abbas, kampuni yao imeshirikiana na baadhi ya taasisi za soka za kubwa ulimwenguni baada ya kuna kuna haja ya kuleta uzoefu huu mkubwa kwa Tanzania.
“Ili kufurahia kuona moja ya klabu kubwa za mpira wa miguu Ulaya, Sevilla FC. Kwa makubaliano yetu na LaLiga ambayo ni ligi bora duniani, tutaweza kuonyesha vipaji vyetu na kuboresha kiwango cha soka nchini “, alisema Talimba.
Alisema kwamba mechi hiyo ni sehemu ya mradi wa ‘LaLiga duniani ambao unalenga kueneza soka la Hispania kimataifa na kueneza pia sera ya ‘Marca España’, kuleta karibu mashabiki wa LaLiga na kukuza klabu nje ya nchi yetu.
Hii itakuwa ni klabu ya pili Ulaya kufanya ziara Afrika Mashariki, baada ya mwaka 2017 Everton FC kucheza na Gor Mahia nchini Kenya, ingawa sio mara ya kwanza kwa Sevilla kutua katika bara hili kwani mwaka 2015 ilikuwa nchini Morocco ambao ilicheza mechi ya kuajindaa na LaLiga dhidi ya timu ya Hassania Union Sport d’Agadir.