Home Mchanganyiko BENKI ya Amana yatumia zaidi ya Shilingi Milioni 80 kufadhili mashindano ya...

BENKI ya Amana yatumia zaidi ya Shilingi Milioni 80 kufadhili mashindano ya Kuhifadhi Quroan Afrika

0

Meneja Mkuu wa Biashara wa Benki ya Amana, Said Mbarouk kushoto akimkahidhi zawadi ya shilingi milioni 7.5 mshindi wa tatu katika mshindano ya kuhifadhi Qur’an Afrika Shamsidin Hussein Ally kutoka Zanzibar kulia ni Katibu wa Mashindano hayo Alhaj Mussa Mushi (Picha na Suleiman Msuya)

………………………………………………………………..

NA SULEIMAN MSUYA

BENKI ya Amana imetumia zaidi ya Shilingi Milioni 80 mwaka huu kufadhili mashindano ya Kuhifadhi Quroan Afrika yaliyoanda na Taasisi ya Al-Hikma ya jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Masoko Amana Benki, Dassu Mussa wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa kwanza, pili na tatu.

Mussa alisema Benki ya Amana imekuwa ikidhamini shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo mashindano ya kuhifadhi Qur’an yanayoratibiwa na Taasisi ya Al-Hikma.

Alisema wamelazimika kutoa zawadi nono ili kuvutia vijana wengine kushiriki mashindano hayo ambayo yanatambulisha uelewa wa dini kwa jamii.

“Amana Benki imetumia zaidi ya shilingi milioni 80 kufadhili mashindano yalifanyika juzi na matarajio yao ni kuendelea kufadhili siku zijazo,” alisema.

Alisema benki hiyo itaendelea kusaidia jamii ambayo inakuwa na mahitaji na kwamba isije kuonekana kuwa wapo kwa ajili ya waislama pekee.

Alisema mashindano hayo ambayo yalishirikisha nchi zaidi 15 yameonesha kuwa na mafanikio hivyo hawana budi kuendelea kuyasapoti.

Mkuu huyo idara alitoa wito kwa Watanzania kufuangua akaunti katika benki ya Amana ili waweze kufaidika na huduma bora zinazotolewa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Mashindano ya Qur’an Afrika, Alhaj Mussa Mushi alisema wanaipongeza Benki ya Amana kwa kuendelea kufadhili mashindano hayo ya kimataifa.

Mushi alisema mashindano ya mwaka huu yamefana na niyakipekee kwa kuwepo ushindani mkubwa baina ya washiriki.

Alisema matarajio yao ni kuongeza nchi nyingine kwa siku zijazo na ikiwezekana kushirikisha Afrika nzima.

Mushi aliwataja washindi watatu katika mashindano hayo kuwa ni Muhammed Diallo kutoka nchini Senegali aliyekuwa mshindi wa kwanza na kuibuka na kitita cha shilingi million 20.

“Wapili ni Farouk Yakoub kutoka Nigeria aliyejishindia shilingi milioni 12 na Shamsidin Hussein Ally kutoka Zanzibar shilingi milioni 7.5,” alisema.

Mashindano hayo ambayo yamefanyika Mei 19 katika Uwanja wa Taifa yalikudhuriwa na Rais John Magufuli kama mgeni rasmi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Ally Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete, Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeiry na wengine wengi