Home Michezo SIMBA YAICHAPA 2-0 NDANDA FC BADO POINTI MBILI TU WATETEE UBINGWA WA...

SIMBA YAICHAPA 2-0 NDANDA FC BADO POINTI MBILI TU WATETEE UBINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA

0

Na Mwandishi Wetu,
TIMU ya Simba SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa mabao 2-0 Ndanda FC ya Mtwara katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo Simba imefikisha  pointi 88 katika mchezo wao wa 35 wa msimu na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya watani wao wa jadi, Yanga ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
Sasa Simba SC inatakiwa kushinda mchezo wake wa Jumanne dhidi ya Singida United Uwanja wa Namfua ili kutawazwa rasmi kuwa mabingwa tena wa Ligi Kuu.

 Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Patrick Aussems umetokana na mabao ya mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere mwenye asili ya Rwanda ndani ya robo saa ya kwanza ya mchezo.
Kagere aliye katika msimu wake wa kwanza Simba SC tangu asajiliwe kutoka Gor Mahia ya Kenya, alifunga bao la kwanza dakika ya sita kwa shuti akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenzake, Nahodha, John Raphael Bocco ambaye naye alipokea pasi ya beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
Kagere akamvisha kanzu kipa wa Ndanda FC, Diey Makonga kuifungia bao la pili Simba SC dakika ya 11 na bao lake la 22 la msimu, akimalizia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chama.
Ndanda wakaamua kucheza kwa kujihami baada ya bao hilo ili kuizuia Simba SC iliyomkosa nyota wake Mganda, Emmanuel Okwi, jambo ambalo liliwasaidia kumaliza mchezo wakiwa wamefungwa ‘2-0 tu’.