Mstahiki Meya wa
Jiji la Tanga Mustapha Selebosi akisisitiza jambo wakati wa kikao cha
baraza la Madiwani cha kuwasilisha taarifa ya utendaji
wa kata kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi
Kaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi akizungumza wakati wa kikao hicho
Diwani wa Kata ya Maweni Jijini Tanga Calvas akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Diwani wa Kata ya Pongwe Mbaraka Sadi
DIWANI wa Kata ya Mswambweni (CUF) Abdulrahamani akizungumza katika
kikao hicho kushoto ni Diwani wa Kata ya Chumbageni (CCM) Saida Gadafi
Baadhi ya madiwani wakipitia makabrasha wakati wa kikao hicho
Tanga imeeleza namna vitambulisho vya
wajasiriamali vilivyotolewa na Rais John Magufuli vilivyowasababishia
kukosa mapato huku vyanzo vyake vya mapato 15 kufutika na hivyo
kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi wakati wa kikao cha
baraza la Madiwani cha kuwasilisha taarifa ya utendaji
wa kata kilichofanyika Jijini hapa na kusema hali ya Halmashauri imekuwa
mbaya
kutokana na vitambulisho hivyo kugawiwa kwa wafanyabiashara wasi
walengwa.
vinatarajiwa kuliingiza Halimashauri hiyo bajeti ya Bil 15 lakini ugawaji wa
vitambulisho kwa wafanyabiashara wasio stahiki imesababisha kasoro hiyo.
cha kupelekea hali hiyo kimesababishwa na Watendaji wa kata na Mitaa kwa
kushindwa kusimamia kwa ukaribu ugawaji wa vitambulishi hivyo kwa watu wanaostahili
na badala yake wamewagawiwa hata wafanyabiashara wasihusika.
mmetuangusha mmegawa vitambulisho hata kwa wafanyabiashara wasiostahili na
mmefanya hivyo ili kuvimaliza lakini ni athari kwetu hasa Halmashauri hatuna
fedha na miradi mingi itakwama”Alisema Seleboss.
alisema watendaji wamechangia kukwamisha
ukusanyaji wa mapato ambapo yamefikia asilimia 65% huku ikiwa bado mwezi mmoja kumalizika
kwa mwaka wa serikali uishe ilihali angalau ukusanyaji huo ulitakiwa ufikie
80%.
ukosefu huo wa mapato umesababisha Halimashauri hiyo kushindwa kutekeleza
shughuli za kijamii kama usafi wa masoko pamoja na marekebisho ya taa za
barabarani.
wameshindwa kutafsiri nia ya Rais kwani vitambulisho vimetolewa hadi kwa wavuvi
pamoja na wafanyabiashara wakubwa wenye maduka sasa wote wamegeuka na kuwa
wajasiriamali”alisema Mustafa.
akiongelea upande wa leseni za biashara Meya Mustafa alisema kuwa wamepoteza
mapato ya kiasi cha sh Mil 700 zilizokuwa zikusanywe kutokana na maombi ya
leseni hizo lakini sasa wafanyabiashara wengi wamerudisha leseni hizo na kukata vitambulisho vya wajasiriamali.
wake Kaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi alisema kuwa ufinyu wa bajeti
umesababisha miradi mingi ambayo walikuwa wamepanga kuitekeleza kushindwa
kutekelezwa kwa wakati .
tunajipanga kuboresha miundombinu ya shule zetu kwa kujenga madarasa mapya
ukarabati ya vyoo pamoja na madawati ambapo tunafanya kila pale tunapopata
fedha japo kidogo”alisema Possi.
wa wilaya ya Tanga Selemani Zumo aliwataka watendaji wa Jiji kuhakikisha
wanafanyakazi kwa uwadilifu na kujituma pamoja na kujua mipaka ya kazi zao.
haiwezekani watendaji hao wakawa ni sehemu ya migogoro baina yao na viongozi wa
kisiasa ambao wao wapo kwa ajili ya kuhakikisha wanasimami maslahi ya wananchi
ambao ni wapiga kura wao.
akichangia mada katika baraza hilo Diwani wa kata ya Mabawa Mwasabu Ngare
alisema baadhi ya taa za barabarani haziwaki na hali hiyo inaweza kuchangia kwa
kiasi kikubwa ongezeko la vibaka na wananchi kupoteza mali zao.
