GEKUL AWATAKA WAZALISHAJI WA MAUDHUI KUZINGATIA UTAMADUNI WA KITANZANIA
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul leo Februari 14, 2023 jijini Dodoma amefunga Mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma wa Sekta…
Latest updates on ministries, public service, parliament, policy decisions, and national administration.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul leo Februari 14, 2023 jijini Dodoma amefunga Mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma wa Sekta…
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani WAHAMIAJI haramu wawili raia wa Nigeria na Cameroon wamekamatwa Mapinga Kibosha, Mkoani Pwani kwa kosa la kuishi nchini kinyume cha…
Mkuu wa Mkoa huo Balozi Dkt Batilda Burian wa Tabora akizungumza na wakulima wa zao la Tambaku wilayani Sikonge mkoani hapa . Mkuu wa…
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Richard Mwangoka ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha kahawa cha GDM cha Mlowo mkoani…
Afisa Elimu Mkoa wa Rukwa Samson Hango akifungua mafunzo kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa huo yahusuyo uboreshaji wa ufundishaji na ujifunzaji wa darasa…
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya uchukuzi na biashara Iringa LTD, Caroline Mwakabungu akizungumza na waandishi wa habari juzi ofisini kwake kumuomba Rais Samia Suluhu…
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas alipotembelea na kukagua kiwanda cha kukoboa Kahawa cha DAE LTD mjini Mbinga shehana ya kahawa iliyokobolewa…
Jengo la maabara katika kituo cha afya Matiri Halmashauri ya wilaya Mbinga mkoani Ruvuma. Na Muhidin Amri, Mbinga HALMASHAURI ya wilaya Mbinga mkoani Ruvuma,imetumia Sh.milioni 500 kutoka mapato ya ndani kujenga kituo cha afya Matiri kata ya Matiri ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wake wa kusogeza na kuimarisha huduma za afya kwa jamii. Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo George Mhina amesema,fedha hizo zimetumika kwa ajili ya kujenga majengo matano ambayo ni jengo la wagonjwa wa nje(OPD)maabara,jengo la wazazi, jengo la kufulia na kichomea taka ambalo ujenzi wake utaanza hivi karibuni. Amesema,ujenzi wa majengo hayo umekamilika kwa asilimia zaidi ya 90 na Halmashauri imepanga kuanza kutoa huduma angalau za awali mapema mwezi April. Mhina amesema,kwa sasa kazi inayofanyika ni kutambua watumishi watakaokwenda kufanya kazi katika kituo hicho,kuleta madawa na vifaa tiba pamoja na usajili wake. Amesema,Halmashauri ya wilaya Mbinga kupitia mapato yake ya ndani imejipanga kuhakikisha vijiji na kata zote kuna vituo vya kisasa vya kutolea huduma ili wananchi ambao ndiyo wanufaika wanafurahia na kwenda kwenye vituo vya serikali kupata huduma mbalimbali za matibabu. Mkazi wa kijiji cha Matiri Joseph Ndunguru amesema, kujengwa kwa kituo hicho cha afya ni ukombozi mkubwa kwao kwani sasa wanategemea zahanati ndogo ambayo kutokana na idadi ya watu waliopo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo baadhi ya dawa,vifaa tiba na watumishi. Nduguru ameiomba serikali,kupeleka vifaa ili ujenzi ukamilike haraka na waweze kupata huduma zote za matibabu karibu, badala ya kuendelea kufuata baadhi ya huduma Hospitali ya wilaya Mbinga kilomita 50 na Hospitali ya St Joseph Peramiho iliyopo umbali wa km 100. Kwa upande wake fundi anayejenga kituo cha afya Matiri Juma Kombo amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zinazotumika kujenga na kuimarisha huduma za afya nchini.…
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa wilaya ya Songwe kwenye ukumbi wa Chuo cha Uuguzi Mwambani uliopo Mkwajuni mkoani Songwe, Baadhi ya watumishi…
Zahanati ya kijiji cha Luwaita Halmashauri ya Mji Mbinga ambayo inasubiriwa kuanza kuhudumia wananchi wa kijiji hicho na kata ya Luwaita ili kuwapunguzia changamoto ya kwenda hadi Hospitali ya wilaya Mbinga mjini umbali wa km 7 kufuata huduma za matibabu. Na Muhidin Amri, Mbinga BAADHI ya wananchi wa kata ya Luwaita Halmashauri ya mji Mbinga wilayani Mbinga,wameiomba serikali kupitia Halmashauri ya Mji Mbinga,kukamilisha ujenzi wa zahanati ya Luwaita kutokana na ujenzi wake kuchukua zaidi ya miaka 5 bila kukamilika. Wamesema kukosekana kwa huduma za afya katika kata hiyo,kumesababisha akina mama wajawazito kulazimika kujifungulia njiani kutokana na vituo vya afya vilivyopo kuwa umbali wa zaidi ya kilomita 7 kutoka katika maeneo wanayoishi. Wameiomba Halmashauri ya mji Mbinga ,kuwahurumia kutokana na mateso wanayopata kutumia muda mwingi kwenda kupata huduma maeneo mengine kwa kuanza mchakato wa kufungua na kutoa baadhi ya huduma katika zahanati hiyo ambayo sehemu kubwa ujenzi wake umekamilika. Bosco Komba amesema, zahanati hiyo ilianza kujengwa kwa muda mrefu kwa wananchi kuchangia nguvu zao ili waweze kupata huduma za matibabu karibu,hata hivyo wanashangazwa na ukimya wa serikali kushindwa kufungua na kutoa huduma kwa wananchi. Maria Nchimbi amesema,wananchi wa kata ya Luwaita wanatamani kuona zahanati hiyo ikianza kutoa huduma kwani wamechoka kuvumilia kutembea umbali mrefu kila wanapohitji kupata huduma za matibabu ambazo zinapatikana kwenye vituo vilivyopo mbali na makazi yao. Mtendaji wa kijiji cha Luwaita Rehema Ameir ameeleza kuwa,awali mpango wa serikali ulikuwa kituo cha afya,lakini kukosekana kwa nguvu kazi za wananchi ikaamua iwe zahanati kwa kuwa zilihitajika nguvu za pamoja kati ya serikali na wananchi wa eneo husika. Hata hivyo amesema,ujenzi wa zahanati ya Luwaita umekamilika kwa asilimia 99 na wakazi zaidi ya 4,000 wanatarajia kupata huduma mara itakapoanza kutoa huduma,lakini kuchelewa kufunguliwa kunatokana na kukosekana kwa vyoo na kichomea taka. Amesema,zahanati hiyo itarahisisha upatikanaji wa huduma na kuwaondolea wananchi adha ya kusafiri umbali mrefu kwenda kutafuta huduma kwenye vituo vingine vya afya na kupunguza muda mwingi wanaopaswa kujikita katika shughuli za maendeleo. Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya mji Mbinga Dkt Maximo Magehema amesema,kimsingi zahanati hiyo imekamilika na serikali ipo katika hatua ya mwisho kuanza kutoa huduma na kuwaomba wananchi kuwa wavumilivu wakati serikali ikikamilisha mambo muhimu ya kiutendaji ikiwamo vifaa na watumishi. Amesema,serikali ya awamu ya sita kupitia Halmashauri ya mji Mbinga imejipanga kuhakikisha kila kijiji kina zahanati na kata kituo cha afya ili kusogeza na kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake.