Wednesday, November 25, 2026

Alex Sonna

Latest updates on ministries, public service, parliament, policy decisions, and national administration.

26397 Stories
PATA MKWANJA X1000 YA DAU LAKO NA KASINO YA MTANDAONI

PATA MKWANJA X1000 YA DAU LAKO NA KASINO YA MTANDAONI

Aprili ya Kishua unaambiwaje jisajili Meridianbet upate mizunguko 50 ya bure kucheza sloti ya kasino ya mtandaoni. Kujisajili bonyeza hapa: https://a.meridianbet.co.tz/c/K0aPCC Furahia sloti mpya…

MAJALIWA: MADAWATI 1,393 YAMEUNDWA KUPINGA UKATILI

MAJALIWA: MADAWATI 1,393 YAMEUNDWA KUPINGA UKATILI

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeunda madawati 1,393 ya ulinzi na usalama wa mtoto katika shule za msingi na sekondari ili kupinga ukatili dhidi ya…

WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI MBAWALA WAISHUKURU RUWASA KUMALIZA KERO YA MAJI

WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI MBAWALA WAISHUKURU RUWASA KUMALIZA KERO YA MAJI

  Baadhi ya wanafunzi wa hule ya Sekondari Mbawala Halmashauri ya wilaya Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja na Mhandisi Aloyce Milyangula wa kwanza mstari wa nyuma kutoka ofisi ya meneja wa Ruwasa wilaya ya Nanyumbu. Mwanafunzi wa kidato cha pili Fatma Hamis akichota maji katika kituo kinachotoa huduma ya maji kilichojengwa  shuleni hapo.  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mbawala Halmashauri ya wilaya Mtwara wakifurahi huduma ya maji baada ya Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira(Ruwasa)kufikisha huduma ya maji katika shule hiyo. Muhidin Amri, Mtwara KERO kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Mbawala Halmashauri ya wilaya Mtwara mkoani Mtwara kutembea zaidi ya kilomita mbili kwenda kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya kila siku shuleni hapo imebaki kuwa Historia. Kero hiyo  imemalizika baada ya wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) wilaya ya Mtwara kufikisha mtandao wa maji ya bomba katika shule hiyo. Wanafunzi wa shule  walisema,hapo awali walipata wakati mgumu katika masomo yao kwani  kabla ya kuingia madarasani kuanza masomo walilazimika  kwanza kwenda kutafuta maji yanayopatikana kwenye mabonde  ama kuchimba mashimo kwa mikono hali iliyosababisha kukosa baadhi ya vipindi. Akizungumza kwa niaba ya wenzake mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule hiyo Fatma Hamis alieleza kuwa,kukosekana kwa maji safi na salama kulisababisha mazingira ya shule kuwa machafu na wanafunzi kwenda shule wakiwa wachafu. Aidha alisema,baadhi ya wanafunzi wameamua kuacha masomo ili kuepuka usumbufu  wa kutembea umbali mrefu kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya shule hasa usafi wa vyoo na mazingira kwa ujumla. Fatuma,ameishukuru serikali kupitia Ruwasa kutekeleza mradi huo ambao umewezesha kupata muda mwingi wa kujisomea na kuepukana na magonjwa mbalimbali kama kichocho na magonjwa mengine yanayotokana na uchafu. “miaka yote miwili tulisoma kwa shida sana  kutokana na  ukosefu wa maji safi na salama,tulilazimika kwenda kuchota maji yaliyojaa matope kwenye visima vya asili na mbaya zaidi maji hayo yalikuwa machafu na yasiofaa kwa matumizi ya binadamu kwa ajili ya matumizi ya kila siku”alisema. Mwalimu wa zamu Bakari Rajabu alisema,tangu shule hiyo ilipoanzishwa miaka kadhaa changamoto kubwa ilikuwa  ukosefu wa huduma ya maji ambapo wanafunzi  walilazimika kutembea kilomita mbili hadi tatu kwenda kutafuta maji ili yatumike kwa shughuli za usafi na shughuli nyingine muhimu. Alisema,hali hiyo ilisababisha mahudhurio madogo kwa wanafunzi ambao wakati mwingine kabla ya kuingia madarasani walilazimika kwenda kutafuta maji  yanayopatikana mbali na eneo la shule, hivyo kusababisha wanafunzi kuchelewa vipindi vya masomo  na hata kuathiri kazi ya ufundishaji. Mwalimu Rajabu alisema baada ya kupata mradi wa maji safi na salama,mahudhurio ya wanafunzi yameongezeka na kuishukuru serikali ya awamu ya sita kujenga mradi huo ambao umesaidia sana kuinua taaluma na kuongezeka kwa mahudhurio ya wanafunzi. Kwa upande wake Mhandisi wa maji  kutoka ofisi ya Meneja wa Ruwasa wilaya ya Mtwara Aloyce Milyangula alisema,Ruwasa imelazimika kujenga mradi huo ili kutatua tatizo la  upatikanaji wa huduma  iliyokuwepo kwa muda mrefu na kusababisha kutokea kwa magonjwa ya milipuko ya mara kwa mara. Alisema,shida ya maji ilipelekea hata kusua sua kwa shughuli mbalimbali za uzalishaji kwa kuwa wananchi walilazimika kutumia muda mwingi kwenda kutafuta maji kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku badala ya kufanya kazi za kujiletea kipato katika familia zao. Alisema,baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo wananchi wamehamasika kwa kuvuta maji majumbani ambapo hadi tayari zaidi ya kaya kumi zimeingiza maji kwenye nyumba zao na wengine wakiendelea kuleta maombi ili kupata huduma ya kuunganishiwa maji majumbani. Kwa upande wake Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mtwara Anastanzia Wambura, amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza mazingira na vyanzo vya maji ili miradi inayojengwa iwe endelevu  kwa faida ya kizazi cha sasa na kinachokuja.…

WAZIRI MKUU: TANZANIA KINARA MASUALA YA MAAFA

WAZIRI MKUU: TANZANIA KINARA MASUALA YA MAAFA

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kusaini mkataba wa kuanzisha Kituo cha Huduma za Binadamu na Operesheni za Dharura cha…

DK.MWINYI AMEKABIDHIWA TUNZO MAALUM

DK.MWINYI AMEKABIDHIWA TUNZO MAALUM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akipokea Tunzo maalum ya VIP Global Water  Changemarkers Awards,kutoka kwa Rais…

MTATURU APAZA SAUTI BUNGENI.

MTATURU APAZA SAUTI BUNGENI.

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ametaka serikali itoe kauli kuhusu wazee walio zaidi ya miaka 60 kufanya shughuli za vijana ikiwemo kutengeneza barabara…