Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),Ummy Mwalimu (kushoto) akifunua kitambaa kwa kushirikiana na Mkuu wa Mauzo wa Vodacom Tanzania PLC Kanda ya Kati, Grace Chambua (wa kwanza kulia) kuashiria uzinduzi rasmi wa bustani ya msitu wa miti ya kupandwa eneo la Medeli Jijini Dodoma jana, Jiji limetenga eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 10 kwa ajili ya msitu huo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),Ummy Mwalimu akipanda mti kwa kushirikiana na Meya wa Jiji la Dodoma, Prof David Mwamfupe wakati wa kuzindua msitu wa miti ya kupandwa uliopo eneo la Medeli Jijini Dodoma jana ,kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa Mauzo wa Vodacom Tanzania PLC Kanda ya Kati, Grace Chambua
Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC wakiongozwa na Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Kati, Grace Chambua (katikati) Emanuel Medukenya (kushoto) na Ibrahim Salumu (kulia) wakishirikiana kupanda mti eneo la Medeli Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa msitu huo wa miti ya kupandwa wenye ukubwa wa ekari 10.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC wakiongozwa na Mkuu wa Mauzo wa kanda ya kati,Grace Chambua (katikati), Emanuel Medukenya (kushoto) na Ibrahim Salumu (kulia) wakibeba mti kwa ajili ya kupanda eneo la Medeli Jijini Dodoma kwenye msitu wa miti ya kupandwa ,miti hiyo ilipandwa jana wakati wa uzinduzi rasmi wa msitu huo.