Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Fred Abel ambaye ni Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha Nyamhongolo jijini Mwanza kuhusu picha ya muonekano wa Kituo hicho kitakapokamilika, Desemba 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi cha Nyamhongolo jijini Mwanza, Desemba 17, 2020. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na wa tatu kulia ni Mhandisi Mshauri wa Mradi huo, Mhandisi Fred Abel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Jengo la Kituo cha Mabasi cha Kisasa cha Nyamhongolo kinachojengwa jijini Mwanza ambacho Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake, Desemba 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Picha inayoonyesha muonekano wa Kituo cha Mabasi cha Nyamhungolo kinachojengwa jijini Mwanza ambacho Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake, Desemba 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). Jengo la Hosteli ambalo ni moja kati ya majengo yanayojengwa katika Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kisasa cha Mabasi cha Nyamhongolo jijini Mwanza ambacho Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake, Desemba 17, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)