Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ibenzi Ernest akimuongoza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe (aliyevaa kaunda
suti) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, Dk. Doroth Gwajima (wa tatu kulia) kwenda kuzindua ukarabati wa chumba cha dharula na
uangalizi wa wagonjwa mahututi (ICU),
wakati wa maadfhimisho ya miaka 100 tangu Hospitali hiyo hiyo ianzishwe
1920. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe (wa pili kushoto ) akikata utepe kuzindua rasmi ukarabati wa chumba cha dharula na uangalizi wa
wagonjwa mahututi (ICU), katika Hospitali hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, Dk. Doroth Gwajima.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe akikagua chumba cha
uangalizi wa wagonjwa mahututi (ICU).
Jengo la Wazazi
Jengo la Bima ya Afya
Wanafunzi wa Chuo cha Afya Mirembe, mkoani
Dodoma wakitumbuiza kwa wimbo maalumu wakati wa maadhimisho hayo.
Sehemu ya wafanyakazi na wageni waalikwa
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, Dk. Doroth Gwajima akitoa neno wakati wa maadhimisho hayo.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akitoa ahadi ya kujenga choo na bafu eneo la wananchi wanaosubiria wagonjwa wao katika Hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Meja mstaafu John Salingo akielezea kuwa mafanikio ya Hospitali hiyo ni Utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Baadhi ya watumishi na wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho hayo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Best
Magoma akitoa nasaha zake wakati wa maadhimisho hayo.
Aliyekuwa Muuguzi Mkuu wa Mkoa Anatolia Mkindo akikabidhiwa cheti cha
kutambua mchango wake katika hospitali hiyo kabla ya kustaafu. Baadhi ya watumishi wa hospitali waliostaafu
walitunukiwa vyeti.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali hiyo, Dk.
Ezekiel Mpuya akimkabidhi tuzo maalumu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Profesa Mabula Mchembe.
Happy Mwaikugile ambaye ni mmoja wa wafanyakazi bora akilakiwa kwa furaha na wafanyakazi wenzie baada ya kutunukiwa tuzo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Mabula Mchembe (kulia) akimkabidhi tuzo
maalumu Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ibenzi
Ernest kwa uongozi wake thabiti.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Best
Magoma akitoa nasaha zake wakati wa maadhimisho hayo.