*************************************
Ripoti ya ECDC iliyochambuliwa na shirika la habari DW, inaonesha kwamba Tanzania ni Taifa pekee duniani lisilokua na maambukizi ya maradhi ya COVID-19.
Kwa mujibu wa DW, utafiti huo wa kitaalamu zaidi ulimwenguni umefanyika ndani ya siku 14 zilizopita.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mataifa yaliyoendelea ndio yanayoongoza kwa maradhi hayo hatari. Watu wengi kwenye mataifa hayo huamini kwenye weledi wao wa sayansi na teknolojia huku wakikanusha uwepo wa Mwenyezi Mungu.
Mafanikio haya yametokana na kitendo cha raia wa Tanzania kuamini kwamba Mwenyezi Mungu ndiye mwenye uwezo wa kuyaangamiza maradhi hayo ambayo yameshindikana kutokomezwa kwenye mataifa yaliyoendelea.
Ikumbukwe kwamba, mara baada ya maradhi hayo kuingia nchini, Mhe. Rais Mwl. Dkt. John Magufuli aliwaomba raia watanzania wafanye maombi ili Mwenyezi Mungu ayaangamize maradhi hayo huku akihimiza matumizi ya tiba asilia.
Tunamshuru sana Mwenyezi Mungu kwa kujibu maombi yetu.