……………………………………………………………………….
Na John Walter-Manyara
Mwili wa aliyekuwa Padri wa Shirika la Wapalotini Padri Victor Sanka umepumzishwa Leo agosti 28,2020 katika makaburi ya Wapalotini yaliyopo katika Parokia ya Galapo wilaya ya Babati Mkoani Manyara.
Padri Victor Sanka amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.
Sanka ambaye ni mzaliwa wa Kijiji cha Bashnet wilayani Babati Mkoa wa Manyara, ni kati ya walelewa wa kwanza waliojiunga na shirika la Wapalotini.
Askofu wa Jimbo Katoliki Mbulu Antony Lagwen amewaambia mamia ya waombolezaji waliofika katika ibada ya kumsindikiza kwenye nyumba ya milele, wamuenzi Padri Sanka kwa kutenda yale yaliyo mema.
Padri Sanka alifariki dunia agosti 22,2020 katika hospitali ya Buma iliyopo Bashnet alipokuwa akipatiwa matibabu.
Raha ya ya milele umpe ee Bwana, Mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa Amani,Amen.