Mkurugenzi wa miradi wa shirika la World Vision Tanzania akitoa taarifa ya mradi wa Katerero AP kwa mgeni rasmi pamoja na wananchi waliojitokeza kwenye hafla ya kuufunga mradi huo.Mgeni rasmi Katibu tawala wilaya ya Bukoba Kadore Kilugala akihutubia kwaniaba ya mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro kwenye hafla ya kufunga mradi wa Katerero AP.Mratibu wa mradi wa Katerero AP Atugonza Kyaruzi akitoa ufafanuzi wa namna wananchi walivyonufaika na mradi wa Katerero AP Kwa wananchi na Mgeni Rasmi.Wanavikundi walionufaika na mradi wa Katerero AP Wakimuonyesha baadhi ya bidhaa mgeni Rasmi wanazoshughulika nazo baada ya kusaidiwa na shirika la World Vision.Wanafunzi wa shule ya msingi Katerero wakitoa burudani kwenye hafla ya kufunga mradi wa Katerero AP unaofadhiliwa na shirika la World Vision Tanzania.
*************************************
Na Allawi Kaboyo Bukoba
Shirika lisilo la kiserikali la World Vision Tanzania limetumia Zaidi ya shilingi Bilion 12 kwa miaka 17 kuendesha miradi mbalimbali katika mradi wao mkuu uliojulikana kama Kaerero AP halmashauri ya wilaya Bukoba mkoani Kagera Kwa kuwanufaisha wananchi 28,671
Akiongea katika hafla ya kuufunga mradi huo iliyofanyika Agost 26, mwaka huu na kuhudhuliwa na Katibu tawala wa wilaya ya Bukoba Kadole Kilugala aliyekuja kwaniaba ya mkuu wa wilaya hiyo pamoja na baadhi ya wananchi wanufaika wa mradi Mkurugenzi wa miradi shirika la world vision Tanzania John Masenza alisema,mradi wa kata Katerero umeweza kuhudumia vijiji 10 na kata nne ambapo umenufaisha watu 39090 huku wanufaika wa moja kwa moja wakiwa 28,671.
Masenza alisema,wanufaika hapa wameweza kujifunza shughuli za kilimo, ufugaji ,ujasiriamali, uboreshaji wa afya maji na elimu na kugarimu shilingi bilioni 12.7 kwa muda wa miaka 17 ya mradi huo.
Hata hivyo alisema kuonekana kwa mafanikio hayo ni kwa ushirikiano wa Serikali na shirika kwa ufadhili wa nchi ya Australia iliyokuwa ikitoa pesa ya huduma hizo.
Katibu Tawala wa wilaya Bukoba Kadole Kilugala alisema,ujuzi uliojengwa kwa wananchi wa kata nne ndani ya wilaya hiyo,itasaidia kuwafaa kipindi chote ambacho shirika halitakuwepo.
“Tambueni mtu anaekupa ujuzi wa Jambo la kujitegemea Ni mzuri kuliko yule anayekupa leo alafu kesho usimwone tena niwaambieni ujuzi huu utumieni nyakati zote shirika linapokuwa halipo“alisema Kilugala
Vile vile Kilugala alisema, mashirika yanayoleta ufadhili kwa jamii yanasaidia kuongeza msukumo wa maendeleo kwani yanaweka mchango wake kwa Serikali kusaidia jamii ambayo inauhitaji muhimu.,
BAADHI ya Wananchi wa kata katerero wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wameiomba Serikali kuwapatia ufahamu wa jinsi ya kuendesha miradi ya maendeleo kwa jamii inayoanzishwa na Serikali pamoja na wafadhiri mbalimbali ili kuleta matokeo chanya yatokanayo na miradi hiyo.
Walisema ufahamu huo utasaidia kuongeza sehemu ya kuelewa shughuli inayoletwa kwa jamii Kama namna ya kusaidia katika uzalishaji mali ndani ya sekta mbalimbali ambapo mradi huo ulikuwa ukihudumu kwenye kata za Katerero,Bujugo, Kanyangereko na Kemondo.
Johanes Joel mkazi wa kata Katerero alisema, miradi inayoletwa inawalenga wananchi kuwabadilisha kwenye maisha na kupiga hatua ya maendeleo kwa kile kinachokusudiwa.
“Bila kupewa kwanza ufahamu inakuwa vigumu kuyafanya na kuonyesha mwitikio kwani hatuna mwanga wa kuendesha wenyewe na kupata kitu chanya”alisema Joel
Jeneroza Hamlungi mkazi wa kijiji Burinda kata Bujugo alisema,kuwa na wingi wa miradi inategemewa wananchi kupewa elimu ya kufahamu jambo na kutoka kwenye utegemezi wa ndugu na Serikali.
Aidha alisema idadi kubwa mashirika yanatoa elimu wezeshi kwa jamii kabla ya kuwapatia mradi na hukakikisha kundi linasimama lenyewe na kunufaika Kama wanavyotegemea .
“Jamii inamwitikio endapo itatambua kile kinacholetwa kinahitaji nini kwa Jami na kufundisha na kufikia wengine wengine kutoa kwenye umasikini mi napongeza mashirika “alisema Hamlungi.
Sharifa Kakulwa mwenyekiti wa Kamati ya maendeleo ya Jamii kata Katerero alisema kupitia shirika la world vision wananchi wameweza kuunda vikundi zaidi ya 300 ambavyo vinanufaika na uchumi, kilimo,afya, elimu, maji.
Aliongeza kuwa,kundi la wanawake limeamka na kujiamini kuanzisha uzalishaji ambao unawapatia kipato na kuendesha maisha yao tofauti na hapo awali.