Makamu wa Rais – Mh. Samia Suluhu akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB – Benedicto Baragomwa ni jinsi gani benki hiyo inavyoisadia sekta ya kilimo nchini, alipotembelea banda lao katika maonesho ya Nane Nane Mkoani Simiyu. Katika kuendeleza kilimo na kuwainua wakulima, mwaka huu NMB imetenga TZS bilioni 1.9 zitakazotumika kwa ajili ya kujenga maghala ya kuifadhia mazao eneo ambalo Serikali imetenga.
Afisa Ushirika wa NMB Foundation – Expedito Nyakunga, akitoa maelezo ya namna ya kumiliki Trekta kwa wananchi waliotembelea banda la NMB kwenye maonesho ya Nane Nan yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.Wakulima wakipata elimu ya kibenki na AgriBiashara katika banda la NMB kwenye maonesho ya Nane Nane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.