……………………………………………………………………………..
Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Serikali yajiimarisha katika utoaji huduma bora kwa wananchi kwa kuanzisha maabara itakayosaidia kujua ubora wa maji kabla ya kusambazwa kwa wananchi .
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wizara ya Maji Prof. Kitala Mkumbo katika uzinduzi wa maabara ya maji .
Aidha Prof. Mkumbo amesema kwa maabara hiyo itumike kuboresha huduma za maji kwa wananchi ili kuleta manufaa kwa watanzania
.Naye naibu katibu mkuu wizara ya maji Mhandisi Anthony Sanga ametoa wito kwa taasisi za elimu na makampuni ya sekta binafsi kuja kupata ujuzi kupitia maabara hiyo ili kujiimalisha zaidi katika taaluma zao na utoaji wa huduma kwa wateja
Kwa upande wa mkurugenzi wa rasilimali za Maji George Lugomela amesema kuwa wamejiimalisha vyema ili kutoa huduma bora kwa wananchi na wateja kwa ijumaa.
Huku Mhaidrojia Emanuel Nahizi Ameeleza kua maabara hiyo inaweza kujua ubora wa maji kwa kutambua maji hayo yana nini na kutibiwa kabla ya kusambazwa kwa wananchi kwa matumizi ya kibinadamu