Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Idrisa Kisaka, akitoa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo kwa kipindi cha Aprili hadi Septemba 2026, leo. Picha na Baltazar  Mashaka
………………

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesaidia Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kudhibiti na kukusanya zaidi ya sh. milioni 107.15 za madeni ya mapato ya ushuru wa huduma yaliyokuwa yakidaiwa kutoka kwa kampuni zilizokuwa zikitoa huduma katika halmashauri hiyo.

Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Idrisa Kisaka, alisema hayo jana wakati akitoa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo kwa kipindi cha Aprili hadi Septemba 2026, akieleza kuwa awali halmashauri hiyo ilikuwa ikifuatilia madeni ya sh. milioni 92.3 yaliyotokana na kampuni hizo kushindwa kulipa ushuru wa huduma.

Alisema kupitia ushirikiano kati ya TAKUKURU na halmashauri hiyo, kiasi cha zaidi ya sh. milioni 107.15 kilifanikiwa kukusanywa, sawa na zaidi ya asilimia 100 ya deni lililokuwa limefahamika awali.

Kisaka alieleza kuwa ongezeko la kiasi kilichokusanywa lilitokana na uchunguzi wa TAKUKURU kubaini kuwa baadhi ya wafanyabiashara walikuwa wamewasilisha taarifa zisizo sahihi kuhusu madeni yao, hali iliyosababisha kubainika kwa deni jingine la sh. milioni 14.85 juu ya kiasi cha awali cha sh. milioni 92.3.

Katika hatua nyingine, alisema TAKUKURU Wilaya ya Sengerema imefanikisha Halmashauri ya Wilaya hiyo kununua boti mpya ya kisasa aina ya 7M Fiber Boat yenye injini ya nguvu farasi 40 (40HP), baada ya kufanya uchambuzi wa mfumo wa usimamizi wa utoaji leseni na vibali vya uvuvi.

Alisema uchambuzi huo ulifanyika katika Mwalo wa Kata ya Chifunfu na kubaini kuwa halmashauri hiyo haikuwa na boti yake ya doria, hali iliyosababisha maofisa uvuvi kutumia boti binafsi za wavuvi wanapotekeleza operesheni za kudhibiti uvuvi haramu.

Kwa mujibu wa Kisaka, hali hiyo ilisababisha mgongano wa maslahi na kudhoofisha usimamizi wa shughuli za uvuvi, kwa kuwa maofisa hao walikosa uhuru wa kutosha kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wavuvi waliokiuka taratibu na sheria za sekta hiyo.

Aidha, alisema katika kipindi hicho TAKUKURU ilisaidia kudhibiti na kuhakikisha malipo ya jumla ya sh. milioni 15.35 yanafanyika baada ya kuchambua mfumo wa usimamizi na uendeshaji wa Chombo cha Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CSBO) cha KIYAYI wilayani Magu.

Alisema uchambuzi huo ulibaini changamoto mbalimbali, zikiwemo watumishi kutolipwa mishahara kwa wakati, wajumbe wa bodi kutolipwa posho za vikao pamoja na KIYAYI kuwa na deni la huduma ya maji lililokuwa likidaiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA).

Alieleza kuwa kufuatia mapendekezo na maazimio yaliyotolewa, utekelezaji wake umeanza na fedha hizo zimelipwa, ambapo sh. milioni 3.14 zililipwa kama mishahara ya watumishi, sh. milioni 7.13 zikiwa ni malipo ya Ankara ya maji na sh. milioni 5.07 zikiwa ni deni la KIYAYI kwa MWAUWASA.

Katika hatua nyingine, Kisaka alisema TAKUKURU ilifuatilia matumizi ya fedha za miradi 40 ya maendeleo yenye thamani ya sh. bilioni 13.28 na kubaini mapungufu madogo madogo katika utekelezaji wake.

Alisema taasisi hiyo ilitoa mapendekezo ya maboresho ambayo yamefanyiwa kazi na wahusika, hatua inayolenga kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa kuzingatia ubora, thamani ya fedha na malengo yaliyokusudiwa.TAKUKURU YASAIDIA KUKUSANYA SH. MILIONI 107 ZA MADENI MISUNGWI

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesaidia Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi kudhibiti na kukusanya zaidi ya sh. milioni 107.15 za madeni ya mapato ya ushuru wa huduma yaliyokuwa yakidaiwa kutoka kwa kampuni zilizokuwa zikitoa huduma katika halmashauri hiyo.

Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Idrisa Kisaka, alisema hayo leo,  wakati akitoa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo kwa kipindi cha Aprili hadi Septemba 2026, akieleza kuwa awali halmashauri hiyo ilikuwa ikifuatilia madeni ya sh. milioni 92.3 yaliyotokana na kampuni hizo kushindwa kulipa ushuru wa huduma.

Alisema kupitia ushirikiano kati ya TAKUKURU na halmashauri hiyo, kiasi cha zaidi ya sh. milioni 107.15 kilifanikiwa kukusanywa, sawa na zaidi ya asilimia 100 ya deni lililokuwa limefahamika awali.

Kisaka alieleza kuwa ongezeko la kiasi kilichokusanywa lilitokana na uchunguzi wa TAKUKURU kubaini kuwa baadhi ya wafanyabiashara walikuwa wamewasilisha taarifa zisizo sahihi kuhusu madeni yao, hali iliyosababisha kubainika kwa deni jingine la sh. milioni 14.85 juu ya kiasi cha awali cha sh. milioni 92.3.

Katika hatua nyingine, alisema TAKUKURU Wilaya ya Sengerema imefanikisha Halmashauri ya Wilaya hiyo kununua boti mpya ya kisasa aina ya 7M Fiber Boat yenye injini ya nguvu farasi 40 (40HP), baada ya kufanya uchambuzi wa mfumo wa usimamizi wa utoaji leseni na vibali vya uvuvi.

Alisema uchambuzi huo ulifanyika katika Mwalo wa Kata ya Chifunfu na kubaini kuwa halmashauri hiyo haikuwa na boti yake ya doria, hali iliyosababisha maofisa uvuvi kutumia boti binafsi za wavuvi wanapotekeleza operesheni za kudhibiti uvuvi haramu.

Kwa mujibu wa Kisaka, hali hiyo ilisababisha mgongano wa maslahi na kudhoofisha usimamizi wa shughuli za uvuvi, kwa kuwa maofisa hao walikosa uhuru wa kutosha kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wavuvi waliokiuka taratibu na sheria za sekta hiyo.

Aidha, alisema katika kipindi hicho TAKUKURU ilisaidia kudhibiti na kuhakikisha malipo ya jumla ya sh. milioni 15.35 yanafanyika baada ya kuchambua mfumo wa usimamizi na uendeshaji wa Chombo cha Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CSBO) cha KIYAYI wilayani Magu.

Alisema uchambuzi huo ulibaini changamoto mbalimbali, zikiwemo watumishi kutolipwa mishahara kwa wakati, wajumbe wa bodi kutolipwa posho za vikao pamoja na KIYAYI kuwa na deni la huduma ya maji lililokuwa likidaiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA).

Alieleza kuwa kufuatia mapendekezo na maazimio yaliyotolewa, utekelezaji wake umeanza na fedha hizo zimelipwa, ambapo sh. milioni 3.14 zililipwa kama mishahara ya watumishi, sh. milioni 7.13 zikiwa ni malipo ya Ankara ya maji na sh. milioni 5.07 zikiwa ni deni la KIYAYI kwa MWAUWASA.

Katika hatua nyingine, Kisaka alisema TAKUKURU ilifuatilia matumizi ya fedha za miradi 40 ya maendeleo yenye thamani ya sh. bilioni 13.28 na kubaini mapungufu madogo madogo katika utekelezaji wake.

Alisema taasisi hiyo ilitoa mapendekezo ya maboresho ambayo yamefanyiwa kazi na wahusika, hatua inayolenga kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa kuzingatia ubora, thamani ya fedha na malengo yaliyokusudiwa.