Kongamano la Kimataifa la 2026 la Masomo ya Lugha na Utamaduni wa Afrika” limefanyika kuanzia Novemba 24 hadi 25, 2026 katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa, nchini Ethiopia.
Kongamano hilo lenye mada ya “kufunzana kati ya staarabu tofauti na maendeleo na ushirikiano kati ya China na Afrika katika zama mpya,” ambalo ni moja kati ya shughuli muhimu za Mwaka wa Mawasiliano ya Utamaduni kati ya China na Afrika, limeandaliwa kwa pamoja na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Beijing na Chuo cha Elimu na Utafiti wa Lugha katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa, na kushirikisha wataalamu na wasomi kutoka vyuo vikuu na taasisi za utafiti vya China, Ethiopia, Nigeria, Kenya, Afrika Kusini, Falme za Kiarabu (UAE), Benin, na Uingereza.
Washiriki wamekubaliana kwa kauli moja kwamba kongamano hilo limejenga jukwaa la kubadilishana masomo ya kitaaluma lililo wazi, la kivitendo, na anuwai, likisaidia kuimarisha uelewa wa pamoja kati ya taaluma za Kichina na Kiafrika katika maeneo kama lugha na utamaduni, elimu na ufundishaji, masomo ya nchi na ya kikanda, na kukuza utoaji na ushirikishwaji wa pamoja wa matokeo ya utafiti.
