……………………………………………………………………………….
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Y. Ndugai (Mb), anasikitika kutangaza kifo cha
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mhe. Mchungaji Dkt. Gertrude Rwakatare
kilichotokea Jijini Dar es Salaam alfajiri ya leo Jumatatu tarehe 20 Aprili, 2020.
“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe.
Rwakatare. Natoa pole kwa wafiwa wote wakiwemo familia ya marehemu,
ndugu, jamaa, Waheshimiwa Wabunge na Waumini wa Kanisa la Mlima wa
Moto (Mikocheni B Assemblies of God). Mwenyezi Mungu awape moyo wa
uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Mhe. Spika.
Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu inaratibu mipango ya
mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina.