Aliyekuwa Rais wa Sudan, Omar al-Bashir amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza tangu kuondolewa kwake madarakani mwezi Aprili. Bwana Bashir alikuwa akitolewa gerezani katika mji mkuu, Khartoum kwenda kwenye Ofisi ya mwendesha mashtaka ambaye alimsomea mashtaka ya rushwa yanayomkabili.
Akiwa amezungukwa na askari wa usalama, Kiongozi huyo wa zamani mwenye miaka 75 alikua amevaa vazi lake jeupe na kilemba.
Bwana Bashir alipinduliwa madarakani baada ya miezi kadhaa ya maandamano nchini humo.
Kwa mujibu wa BBC. Waendesha mashtaka wanasema kuwa maburungutu ya fedha za kigeni yalikutwa kwenye magunia nyumbani mwake baada ya kuondolewa madarakani alikohudumu kwa takribani miaka 30. Bashir alionekana akishuka kwenye gari kuingia kwenye ofisi ya mwendesha mashtaka, akitabasamu na kuzungumza na walinzi, lakini baadae alirejea akiwa na uso usio na furaha, Shirika la Reuters limeeleza.
Bwana Bashir pia anatakiwa na mahakama ya kimataifa, ICC, akishutumiwa kuongoza vitendo vya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu katika eneo la Darfur, shutuma ambazo amezikana.
Wakati huohuo, Mohamed Hamdan ”Hemeti” Dagolo,ambaye ni makamu wa rais wa jeshi la junta aliahidi kuwafikisha mbele ya sheria watu ghasia za hivi karibuni.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Kwa mujibu wa wanaharakati wa upinzani, zaidi ya watu 100 waliuawa tarehe 3 mwezi Juni vikosi vya Sudan vilimaliza maandamano baada ya waandamanaji kupiga kambi makao makuu jeshi wakidai utawala wa kiraia.
Kwa mujibu wa wanaharakati wa upinzani, zaidi ya watu 100 waliuawa tarehe 3 mwezi Juni vikosi vya Sudan vilimaliza maandamano baada ya waandamanaji kupiga kambi makao makuu jeshi wakidai utawala wa kiraia.