*****************************
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro ametoa muda wa mwezi mmoja kwa wananchi wanaowatumikisha watoto wadogo kazi za majumbani (House Girls) kuhakikisha wanawpaleka watoto hao shule au kuwarejesha makwao
Dc Muro amesema endapo familia zinazoishi na watoto hao wa kazi wakishindwa basi amewataka wawapeleke katika ofisi za Mkuu wa wilaya ya Arumeru ambapo Idara ya ustawi wa jamii italazimika kuwapeleka katika maeneo maalum ya kuwalea ili kuweza kupata fursa ya Elimu na malezi bora