Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa leo Machi 5, 2020 amekabidhi mkopo uliotolea na Benki ya CRDB wa matrekta manane aina ya Mahindra na majembe yake yenye thamani ya sh. Milioni 65 kwa Vyama Vinne vya ushirika vya wakulima wa mkonge mkoani Tanga. Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa moja ya matrekta hayo Emmanuel Urio ambaye ni mkulima. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye shamba la mkonge la wakulima wadogowadogo la Mwelya Sisal Estate la Korogwe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Machi 5, 2020 amekabidhi mkopo uliotolewa na Benki ya NMB wa matrekta 11 na matrela yake 22 yenye thamani ya sh. Bilioni moja, kwa Vyama Vinne vya ushirika vya wakulima wa mkonge mkoani Tanga. Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi ufunguo wa moja ya matrekta hayo Greyson Nyari , Mwenyekiti wa Vyama vya Mkonge Mkoa wa Tanga kwenye shamba la mkonge la wakulima wadogowadogo la Mwelya Sisal Estate la Korogwe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua matrekta manane aina ya Mahindra na majembe yake yenye thamani ya sh. Milioni 65 yaliyotolewa kwa mkopo na Benki ya CRDB kwa kwa Vyama Vinne vya ushirika vya wakulima wa mkonge mkoani Tanga. Mheshimiwa Majaliwa aliyakabidhi matrekta hayo kwa wakulima kwenye shamba la mkonge la wakulima wadogowadogo la Mwelya Sisal Estate la Korogwe Tanga, Machi 5, 2020.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa leo Machi 5, 2020 amekabidhi mkopo uliotolewa kwa mkopo na Benki ya NMB wa matrekta 11 na matrela yake 22 yenye thamani ya sh. Bilioni moja, kwa Vyama Vinne vya ushirika vya wakulima wa mkonge mkoani Tanga. Pichani, Mwenyekiti wa Vyama vya Mkonge mkoani Tanga, Greyson Nyari (wa pili kulia) akionyesha ufunguo wa moja ya matrekta aliyokabidhiwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)