Mkuu wa Itifaki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwasilisha hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati wa sherehe ya kumbukizi ya miaka 60 kuzaliwa Mfalme Naruhito wa Japan na Siku ya Taifa la Japan iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Japan chini Tanzania, Mhe. Balozi Shinichi Goto
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hutuba ya mgeni rasmi wakati wa sherehe ya kumbukizi ya miaka 60 kuzaliwa Mfalme Naruhito wa Japan na Siku ya Taifa la
Japan iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Itifaki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan chini Tanzania, Mhe. Balozi Shinichi Goto
Wanakwaya wa kwaya ya Dar es Salaam wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania pamoja na wa Japan wakati wa sherehe ya kumbukizi ya miaka 60 kuzaliwa Mfalme
Naruhito wa Japan na Siku ya Taifa la Japan iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
****************************
Tanzania na Japan zimeahidiana kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia pamoja na kushirikiana katika kuhakikisha maendeleo katika sekta za biashara, uwekezaji na
viwanda baina ya nchi hizo mbili.
Akihutubia sherehe ya kumbukizi ya miaka 60 kuzaliwa Mfalme Naruhito wa Japan na Siku ya Taifa la Japan kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Mkuu wa Itifaki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge alisema kuwa Tanzania na Japan zimekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia ambapo kutoka na uhusiano, Japan imekuwa ikisaidia ujenzi wa miradi mbalimbali kama vile ujenzi wa miradi ya maendeleo kama vile daraja la juu lililopo eneo la Tazara (Mfugale flyover) na mradi wa umeme wa Kinyerezi II.
“Kutokana na Uhusiano mzuri baina ya Tanzania na Japan serikali ya Japan imefadhili miradi mingine mbalimbali hpa nchini ikiepo ujenzi wa barabara ya Iringa-Dodoma, Dodoma – Babati, Tunduru – Namtumbo, pamoja na upanuzi wa barabara ya Bagamoyo eneo la kuanzia Morocco hadi Mwenge”. Amesema Balozi
Kanali Ibuge.
Balozi Kanali Ibuge aliongeza kuwa, mbali na sekta ya ujenzi, pia Japan imefadhili miradi mbalimbali katika sekta muhimu nchini kama vile elimu, afya, maji na michezo.
“Serikali ya Japan imechangia sana sula la elimu ambapo watanzania (wanafunzi) wengi wamekuwa wakipata ufadhili wa kusomeshwa Japan mafunzo ya muda mrefu
nay ale ya muda mfupi na yamechangia kwa kiasi kikubwa ufanisi wa rasilimali watu,”. Amesema Balozi Kabudi Ibuge.
Kwa upande wake, Balozi wa Japan chini Tanzania, Mhe. Balozi Shinichi Goto amesema kuwa Japan inatambua Tanzania mara baada ya ameishukuru Serikali ya
Tanzania kwa umoja na mshikamano ambao imekuwa ikionesha kwa Japan na kusema kuwa umoja huo umekuwa ni chachu ya maendeleo kwa Tanzania na
Serikali ya Japan.
Japan imekuwa ikifurahia uhusiano wa kirafiki na mzuri na Tanzania kwa muda mrefu sasa, ambapo pamoja na mambo mengine Mhe. Balozi, Goto ameishukuru
Serikali ya Tanzania kwa umoja na mshikamano ambao imekuwa ikionesha kwa Japan tangu wakati huo na kusema kuwa umoja huo umekuwa ni chachu ya
maendeleo baina ya mataifa hayo mawili.
“Urafiki wa kiuchumi kati ya Tanzania na Japan kwa sasa ni imara, na ni matumaini yetu kuwa katika siku za usoni uhusiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Japan utafikia hatua mpya ya ushirikiano”. Amesema Balozi Goto.