Kamanda wa polisi mkoani Arusha ,Jonathan Shanna akionyesha moja ya silaha waliyokutwa nayo majambazi hao
silaha mbalimbali na simu za mkononi walizokutwa nazo majambazi hao baada ya kuuawa wakati wakijiandaa kwenda kufanya uhalifu
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habari Mara baada ya jeshi la polisi kufanikiwa kuwaua majambazi watano mkoani Arusha (Happy Lazaro)
……………………………………………………………………………………….
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Jeshi la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuwauwa majambazi sugu watano baada ya kujibizana na polisi wakati wakienda kufanya uhalifu .
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha,Kamanda wa polisi Jonathan Shanna amesema kuwa,tukio Hilo limetokea januari 29 mwaka huu majira ya saa 3:45 asubuhi katika njia panda ya Mateves kata ya Olmot Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Kamanda Shanna alisema kuwa,tukio hili limetokea baada ya jeshi la polisi kupata taarifa fiche kuwa majambazi hao walikuwa wamepanga kwenda kufanya tukio la ujambazi katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.
Alisema kuwa,majambazi hayo walipanga kutumia barabara ya Afrika Mashariki (Bypass) kupitia Olasiti Hadi mzunguko wa kwa mrombo kwa kutumia usafiri wa pikipiki tatu ambazo walikuwa nazo .
Amesema kuwa,Mara baada ya polisi kupata taarifa hizo waliweka mtego katika njia panda ya Mateves ambapo ilipofika majira ya saa 3:45 usiku Askari hao walionao pikipiki tatu ambazo zilikuwa zinatokea upande wake Mateves kuelekea barabara mpya ya Afrika Mashariki ,ambapo walisimamishwa na Askari hao lakini badala ya kutii amri majambazi hayo walianza kufyetua risasi.
Ameongeza kuwa,baada ya hapo ndipo kikosi kilianza kujibu mapigo ambapo majibizano hayo yalichukua muda takriban dakika 35 , ambapo majambazi wanne walifariki hapohapo huku jambazi mwingine Mmoja aliyekuwa nyuma aligeuza na pikipiki yake na kukimbia umbali was mita 500 lakini naye alipigwa risasi na kudondoka.
Aidha katika eneo la tukio walikuta vitu mbalimbali vilivyokuwa vinatumuwa na majambazi hao ikiwemo pikipiki tatu ambazo ni MC 871 BWR aina ya Skygo ,MC 555 CGE aina ya Kinglion ,MC 478 AYV aina ya Toyo,bunduki moja aina ya Shortgun pump action yenye namba 32265,Chinese Pistol moja iliyofutwa namba zake za usajili ,bastola moja ya bandia.
Alitaja vitu vingine kuwa ni magazine mbili za Chinese ,Pistol moja ikiwa na risasi 8 na nyingine ikiwa na risasi 1 .maganda 7 ya risasi ya Chinese Pistol,risasi 2 za bunduki aina ya Shortgun,maganda 5 ya risasi ya Shortgun na simu mbili aina ya Tecno na moja aina ya Oking.
Aidha alisema kuwa, uchunguzi wa awali umebaini kuwa bunduki hiyo aina ya Shortgun pump Action iliibiwa januari 26,mwaka huu majira ya saa 9:00 usiku nyumbajni kwa Jackson Msangi baada ya majambazi hao kuvunja nyumba yake iliyopo maeneo ya Burka ,kata ya Olasiti.
Amesema kuwa,walifanikiwa pia kuiba simu ya mkewe aitwaye Nikira Msangi ambapo yet na mume wake wametambua bunduki na simu vilivyoibiwa siku hiyo waliyovamiwa.
Aidha miili ya marehemu imehifadhiwa ktika hospitality ya mkoa ya Mount meru kwa uchunguzi wa Daktari na utambuzi.
“Tunatoa onyo Kali kwa watu wote wenye tabia ya kuvuna bila kupanda kuacha tabia hiyo mara moja kwqni hatutasita kuwachukulia hatua Kali za kisheria ,na tunatoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za kihalifu ili tuweze kutokomeza kundi la watu wachache wanaochafua mkoa wetu”amesema Kamanda Shanna..
Naye mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alilipongeza jeshi hilo kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuwaua majambazi hao kwani wangeweza kusababisha madhara makubwa huko walipopangiwa kwenda kufanya uhalifu.
Gambo amesema kuwa,usalama ni kipaumbele chetu na mkoa wa Arusha ni mkoa wa kitalii kwani asilimia 25 ya fedha zinazopatikana zinatokana na utalii,hivyo kuna haja kubwa ya kuimarisha ulinzi kuhakikisha watalii wanakuwa salama muda wote.