MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amemuelekeza kamanda wa polisi mkoa,kumtafuta nabii Elia (shehe Hamza Issa) huko Misugusugu ,Kibaha ili ahojiwe kuhusiana na shughuli hiyo anayoifanya kwa waumini ambao ni wanawake pekee.
Aidha nabii huyo anadaiwa kuishi na mke wa mdogo wake ,Halima Hajji bila ridhaa ya mdogo wake huku akidai anampa maombi .
Akielezea juu ya tukio hilo Ndikilo alibainisha,endapo atabainika kufanya shughuli hizo nje ya imani ya dini ya kiislamu asitishiwe kazi hiyo na sheria ichukuliwe.
“Taarifa zilizotoka kwa mdogo wake ,mkewe aliondoka na mtoto wa kiume Abdillah Chande ,ila tangu mkewe achukuliwe na kaka yake hataki kurudi Moshi na akipiga simu hawapokei wakidai wapo kwenye maombi”
Nae shehe wa wilaya ya Kibaha ,Saidi Mtonda alisema, mwaka uliopita mtu huyo alifika BAKWATA wilaya ya Kibaha kuomba kujitangaza na kupewa fursa ya kuhubiri baadhi ya maeneo.
Alisema, walipokuja kufanya utafiti waligundua uhubiri wake hauhashirii imani na maelekezo ya dini ya kiislamu ambapo walimpiga marufuku.
“Mufti wa Tanzania nae tulimfikishia taarifa hizi na alitoa tamko la kutomruhusu na aache shughuli hizo ,sasa kama amerudia atafuatilia ili sheria ichukue mkondo wake kwani hawawezi kufumbia macho mambo yaliyo nje na imani ya dini hiyo”alisisitiza Mponda.