




…………………………………………………………….
Na Anitha Jonas – WHUSM – Tarangire
Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza awasihi wajumbe wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) kuwa Mabalozi wazuri wa kuitangaza hifadhi ya Tarangire.
Mhe.Shonza amteoa kauli hiyo hivi karibuni jijini Arusha alipokuwa akifanya ziara ya kuwaongoza wajumbe wa Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 40 ya PAPU yaliyofanyika hivi karibuni jijini Arusha kutembelea hifadhi hiyo .
“Naamini mmefurahia kutembelea hifadhi hii,na Tanzania imebarikiwa kuwa na hifadhi nyingi ikiwemo Serengeti,Ngorongoro,Manyara na nyingine nyingi ombi langu kwenu ni mkawe mabalozi wazuri katika nchi zenu kutangaza fursa hii ya utalii yaw a hifadhi ya wanyamapori,”alisema Mhe.Shonza.
Akiendelea kuzungumza baada ya kukamilika kwa ziara hiyo ya kutembelea hifadhi hiyo Naibu Waziri huyo alitoa wito kwa wadau mbalimbali kutoka nchi za Afrika kuja kuwekeza nchini kwani kuna usalama na amani, pia alitoa pongezi kwa uongozi wa PAPU kwa maadhimisho ya miaka 40 na hatua ya ujenzi wa ofisi yao ya Makao Makuu jijini hapo.
Naye Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Tarangire Neema Mollel aliushukuru uongozi wa sekta ya Mawasiliano uliyoandaa mkutano huo kwa kuichagua hifadhi hiyo kutembelewa na wageni hao kutoka nchi mbalimbali kwani anaamini wageni hao watasaidia kuwa mabalozi wa kutangaza hifadhi hiyo yenye utajiri wa miti mingi ya mibuyu na wanyama mbalimbali wakiwemo,Simba,Tembo,Twiga , Ngiri,Swala na mto wenye viboko wengi ambapo samba hutumia eneo hilo kuwinda nyumbu wanapokwenda kunywa maji.
Pamoja na hayo nae Katibu Mtendaji Mamlaka ya Tume ya Usimamizi wa Huduma za Posta kutoka nchini Ghana Bibi.Hamdaratu Zakaria alishukuru viongozi wa Tanzania kwa kuwapa fursa ya kutembelea hifadhi hiyo kwani amefurahia sana kuona wanyama mbalimbali akiwemo Twiga,Tembo, Swala,Mbuni na Ngiri,pia alisema amefurahishwa na utamaduni wa ukarimu kutoka kwa watanzania pamoja hali ya usalama na amani iliyopo.