Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Waziri
wa Viwanda, Biashara na masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Paul Mayom Akech kabla ya kuanza mazungumzo yao. Mazungumzo hayo
yamefanyika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba John Kabudi akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo kati yake na Waziri wa Viwanda, Biashara na masuala ya Afrika Mashariki wa
Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Paul Mayom Akech (kushoto). Mazungumzo hayo yamefanyika
ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019.
Waziri wa Viwanda, Biashara na masuala
ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Paul Mayom Akech, akifafanua
jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baada ya mazungumzo kati yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa Palamagamba John Kabudi.
Mazungumzo hayo yamefanyika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Mhe. Profesa Palamagamba John Kabudi (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo kati yake na Waziri wa
Viwanda, Biashara na Masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe.
Paul Mayom Akech (kushoto). Kulia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe. Mkutano huo ulifanyika katika
ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Mhe. Profesa Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya
pamoja na mgeni wake Mhe. Paul Mayom Akech,Waziri wa Viwanda,Biashara na Masuala
ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini. Kushoto kwa Profesa Kabudi ni
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe akifuatiwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe. Mazungumzo ya viongozi hao yalifanyika katika
ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019.